Wednesday 6 August 2014

Hii ndio siri ya Diamond kutomuacha mamaa yake kila aendapo.
10584511_1649508395274921_1890441585_n

Kwa jinsi Diamond anavyoonekana akiwa na ukaribu sana na mama yake mzazi toka day one, wengi wamejaribu kuhoji sana ni nini hasa siri iliyo nyuma ya ukaribu uliopitiliza wa Diamond kwa mama yake, ila siri iliyopo inarudisha nyuma sana kipindi ambacho Diamond akiwa ndio ana-hustle kutafuta njia ya kutokea katika fani hii ya muziki wa Bongo fleva, kipindi hiko ambacho Tanzania haitambui kabisa kama kuna mwanamuziki anayejiita Diamond Platnumz.
p

Kuna mambo mengi sana ambayo bila msaada wa mama yake mzazi, hivi leo kusingekuwa kuna jina linalowakilisha Bongo huko ugaibuni kama Diamond platnumz, tukio moja ambalo hata Diamond mwenyewe hawezi kusahau katika historia ya muziki wake, ni pale mama yake mzazi alipojitolea pete yake ya dhahabu na kuiuza ili mwanaye ambaye ni Diamond apate hela ya kuingia studio na kurekodi track yake ya kwanza.
10576138_770511582969037_1834689818_n

Naamini ni wazazi wachache sana wanaweza kufanya jambo kama hili, mbali na kupitia vizuizi vingi katika safari yake ya muziki, mama yake mzazi ndio aliyekuwa rafiki wake wa karibu aliyefanikiwa kumuongoza Diamond tena bila kukata tamaa, hadi hii leo kufikia mafanikio aliyonayo ambayo hata Raisi wa nchi yake(mH.Jakaya) hawezi kusahau jina la Diamond pale anapojarbu kuongelea sanaa ya muziki huu wa Tanzania. Ukaribu huo unaweza kuonekana ni umetoka mbali, ni zaidi ya mama, ni mtu ambaye amechangia mafanikio makubwa katika muziki wake.
1524981_665641786790972_1806280682_n

No comments:

Post a Comment