Friday 21 February 2014

Ukraine:Hatimaye makubaliano yapatikana

 

Habari za hivi punde zinaarifu kuwa ofisi ya rais Yanukovych nchini Ukrain imetoa taarifa inayosema kwamba mwafaka umefikiwa katika mazungumzo ya usiku kucha kati ya serikali, upinzani na waakilishi wa Muungano wa Ulaya na Urusi.
Taarifa hiyo hata hivyo haikutoa maelezo zaidi kuhusu makubaliano hayo ingawa ilisema kuwa pande zote zitatia saini makubaliano yenyewe.
Duru zinasema kuwa Rais Yanukovych amekuwa akikabiliwa na shinikizo apange uchaguzi wa mapema pamoja na mageuzi ya kikatiba.
Umoja wa Ulaya umekubali kuwawekea vikwazo viongozi waliopanga ghasia zinazoikabili Ukraine kwa sasa.
Uamuzi huo uliofanyika mjini Brussels, Ubelgiji umejiri baada ya watu kadhaa kuuawa mjini Kiev, katika siku ambayo ilishuhudia umwagikaji mkubwa zaidi wa damu tangu uhuru wa Ukraine zaidi ya miaka ishirini iliyopita.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Italia, Emma Bonino, amesema vikwazo hivyo vinavyojumuisha vya usafiri na kupiga tanji mali za wahusika na kwamba vinawalenga wale waliohusika na mauaji ya waandamanaji.
Ujumbe wa Umoja wa Ulaya mjini Kiev unajaribu kuwapatanisha viongozi wa upinzani na rais Victor Yanukovych ili kuleta amani na pia kushawishi taifa hilo kuandaa mapema uchaguzi uliopangiwa kufanyika mwaka ujao.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Ban Ki-moon amesema hali nchini Ukraine ni ya kutamausha:
Wito huo umetolewa vile vile na waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani John Kerry ambaye ametaka vurugu kusitishwa nchini Ukraine akisema kuwa watu wa taifa hilo wanastahili kuwa na hali bora kuliko kile alichokitaja kuwa maafa na mateso yasiyofaa ambayo yameshuhudiwa katika barabara za mji mkuu, Kiev.
Haijabainika ni watu wangapi waliouwawa katika vurugu za Alhamisi lakini wizara ya Afya inasema tangu Jumanne, watu sabini wameuawa na zaidi ya 570 wamejeruhiwa.

 

Ghana yatoa heshima kwa Komla Dumor

 

Komla na aliyekuwa waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai

Hafla mabli mbali za siku tatu kumuenzi aliyekuwa mtangazaji wa BBC Komla Dumor-aliyefariki ghafla mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 41,zitaanza leo nchini Ghana kabla ya maizko yake.
Baada ya kifo chake,rambirambi zilitolewa kutoka kote dunia na rais wa Ghana,John Mahama,alisema kuwa Ghana imempoteza balozi.




Kama ilivyo desturi nchini Ghana,hafla ya mazishi yake itachukua muda wa siku tatu ikianza na misa ya kuomboleza katika kanisa la Accra Roman Catholic cathedral ambapo wananchi wataruhusiwa kutazama mwili wake.

Umati mkubwa unatarajiwa kuhudhuria.
Jumamosi,wasifu wake utasomwa ukisifia yale aliyofanya nchini mwake. Ibada hiyo itafanyika katika uwanja wa Ikulu ya Ghana Ikifuatwa na ibada ya mazishi itakayohusisha familia yake pekee.
Komla Dumor alikuwa mtangazaji maarufu katika stesheni moja ya redio nchi Ghana kabla ya kujiunga na BBC miaka saba iliyopita na aliweza kufahamika kama mtangazaji wa redio na televisheni mwenye haiba kubwa duniani kote.
Katika kazi yake alipenda kuonyesha watazamaji wake kuhusu bara la Afrika na kuwawezesha kuelewa Afrika kwa kina. Kufuatia kifo chake,aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa,Kofi Annan alisema kuwa Afrika imempoteza mmoja wa talanta zake chipukizi.
Aliongeza kwamba, Komla Dumor alikuwa mtangazaji mwenye kupeana motisha aliyedhamiria kuchimbua ukweli na kutangaza ukweli kila wakati.
Maneno haya yalilingana na yale yaliyotolewa na wabunge wa Ghana siku ya Alhamisi. Katika ibada hiyo,mbunge mmoja alitaja kuwa serikali ilikuwa imekubali kuipa jina barabara moja jijini kama ishara ya kumkumbuka.

 

Ikulu ya Rais Somalia yashambuliwa

 

 

Wapiganaji wa kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia meshambulia Ikulu ya Rais katika mji mkuu Mogadishu.
Umoja wa mataifa unasema umefahamishwa kuwa rais wa nchi hiyo hakujeruhiwa na yu salama na kwamba shambulizi la wanamgambo hao lilitibuka.


Waziri wa mambo ya usalama wa nchi hiyo Abdi Karim Hussein, amesema baadhi ya washambuliaji wamefariki na wengine kukamatwa.
Kundi la Al- Shaabab linalopigana na utawala nchini humo limedai kuhusika na shambulio hilo na kusema makabiliano yangali yanaendelea.
Walianza mashambulizi yao, kwa kutumia gari lililokuwa na bomu ndani yake kwa kuliegesha kando ya ukuta na kisha kuanza kupigana ili kuweza kuingia ndani.
Milipuko mikubwa ilisikika pamoja na milio ya risasi.
Majeshi ya muungano wa Afrika yamekuwa yakipambana na wapiganaji hao na hata kuwafurusha kutoka mji mkuu Mogadishu. Hata hivyo bado wanadhibiti sehemu nyingi nje ya Mogadishu


 

Gavana wa benki Nigeria atimuliwa

 

Gavana wa benki kuu ya Nigeria, Lamido Sanusi amesimamishwa kazi kwa muda akisubiri matokeo ya uchunguzi wa kile kinachosemekana kuwa makosa makubwa katika rekodi za benki.
Bwana Sanusi alizua hisia nchini Nigeria aliposema kuwa Dola Bilioni 20 za mapato yaliyotokana na mafuta hazijulikani ziliko.
Shirika la mafuta la serikali, limekanusha madai kuwa halijawasilisha rekodi zake kuhusu lilivyotumia pesa hizo likisema kuwa madai hayo hayana msingi.
Bwana Sanusi anaheshimika sana nchini Nigeria hasa baada ya kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya benki tangu kuteuliwa kama gavana mwaka 2009
Alitajwa kuwa gavana bora zaidi wa beni kuu mwaka 2010 na jarida la Banker magazine.
Nigeria ni moja ya nchi zenye kuzalisha mafuta kwa wingi duniani lakini sekta hiyo imekuwa ikikumbwa na madai ya wizi na ufisadi.
Mnamo mwezi Februari, bwana Sanusi aliambia kamati ya Baraza la Senate kuwa kati ya Dola Bilioni 67 za kimarekani thamani ya kiwango cha mafuta kilichouzwa kati ya mwezi Januari mwaka 2012 na Julai 2013, dola bilioni 20 bado hazijajulikana ziliko.
Shirika la mafuta la serikali lilisema kuwa madai hayo sio ya kweli na kwamba hayana msingi.
Bwana Sanusi anahudhuria mkutano wa kikanda wa wakuu wa benki kuu nchini Niger. Nafasi yake itachukuliwa na naibu wake Sarah Alade, aliyeandamana naye kwenye mkutano huo.
Rais Jonathan alimuomba Sanusi kujiuzulu mwezi Disemba lakini akakataa.
Rais hana mamlaka ya kumfuta kazi gavana wa benki kuu. Ni bunge pekee linaloweza kufanya hivyo.
Muda wake unapaswa kukamilika mwezi Juni lakini duru zinasema kuwa uamuzi wa kumwachisha kazi kwa muda ni muhimu sana. Taarifa ya Rais ilisema kuwa Sanusi anaachishwa kazi kwa sababu ya kuvunja sheria za benki kuu.

 

Huenda UN ikatuma majeshi yake CAR

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, anasema polisi na wanajeshi 3000 zaidi wanahitajika katika Jamhuri ya Afrika ya kati kuwalinda raia dhidi ya ghasia zinazoendelea.

 

Maelfu ya wanajeshi wa Ufaransa na Umoja wa Afrika wapo nchini humo katika jitihada za kusitisha mapigano yanayoendelea kati ya waasi wa kiislamu,Seleka na wapiganaji wa Kikristo wajulikanao kama Anti-Balaka.
Akizungumza mwishoni mwa ziara yake ya siku tatu, maritibu wa misaada wa Umoja huo wa mataifa, Valerie Amos, amesema ameshtushwa na kiwango cha ukosefu wa usalama.
Mwandishi wa BBC katika Umoja wa Mataifa anasema kuna uwezekano mkubwa kwamba Umoja huo utawatuma wanajeshi wake wa kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, lakini hilo huenda likachukuwa miezi kadhaa na hatua za dharura zinahitajika ili kuthibiti ghasia zinazoenea.

 

Kilichosemwa na Mh.Membe kuhusu Mgogoro wa Mpaka kati ya Tanzania na Malawi

membe 

Tanzania bado ipo kwenye mgogoro na nchi ya Malawi juu ya mpaka halisi wa nchi,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Benard Membe amesema hatma juu ya mgogoro huo inategemewa kutolewa mwezi march.

Hukumu hiyo itaamuliwa baada ya jopo la Usuluhishi litakapokaa na kusikiliza pande zote mbili ambalo litaongozwa na Rais wa zamani wa Msumbiji Joachim Chisano
Kupatikana kwa suluhu ya mgogoro wa mpaka huo kutawatoa hofu wananchi wanaoishi pembezoni mwa Ziwa hilo ambao wamekuwa wakitegemea shughuli za uvuvi wakiwemo wakazi wa kijiji cha Manda Jimbo la Ludewa mkoani Njombe.
Wakazi wa eneo hilo wamesema kwa hivi karibuni tangu kutulia kwa vuguvugu la mgogoro huo wamekuwa wakiendelea shughuli zao za maendeleo kama kawaida ikiwemo uvuvi.

malawi

 

Vichwa vya habari vya magazet ya leo

.  

.