Thursday, 27 March 2014
Bei ya gesi kupanda maradufu Ukraine
Serikali ya mpito ya Ukraine imesema itaongeza bei ya gesi kwa watumiaji wa ndani kwa asilimia 50 zikiwa jitihada za kuhakikisha kuwa wanafanikiwa kupata mkopo kutoka Shirika la fedha duniani, IMF
Ukraine hununua gesi nusu ya gesi yake ya asili kutoka kampuni ya Gazprom ya Urusi, kisha huiuza kwa watumiaji wake kwa gharama nafuu.
IMF halikadhalika inaitaka Ukraine kupambana na vitendo vya rushwa na kusitisha mchakato wa Benki kuu ya Ukraine kusaidia fedha ya nchi hiyo.
Siku ya jumanne, waziri wa fedha wa nchi hiyo Olexander Shlapak alisema Ukraine inahitaji kiasi cha Pauni bilioni 9-12 kutoka kwa IMF.
Jarida la Financial Times limeripoti kuwa uamuzi uko mbioni kufikiwa kuhusu kiasi cha fedha cha takriban dola za kimarekani bilioni 15
ambacho Ukraine inatakiwa kujiokoa na kwamba maamuzi hayo yatatangazwa rasmi Alhamisi.
Makubaliano kati ya Ukraine na IMF ni muhimu wakati huu ili kuweza kupata misaada zaidi kutoka kwa Jumuia ya Ulaya na Marekani.
Msaada wa kifedha unahitajika haraka wakati nchi hiyo ikiwa imelazimika kutumia hifadhi ya fedha za kigeni,huku uchumi nao ukitarajiwa kuanguka kwa 3% mwaka huu.
Wizara ya fedha nchini humo pia inatarajia msaada kutoka kwa Marekani japo kiasi kamili kinasubiri mjadala na bunge la Congress.
Rais Uhuru na naibu wake walipoamua kusimamisha msafara ili kula.
Ni picha ambayo nimetumiwa na Mwandishi wa habari wa Kenya ikimuonyesha Uhuru Kenyatta ambae ni Rais wa nchi hiyo akiwa na naibu wake William Ruto baada ya kuamua kusimama njiani wakitokea Arusha kwa gari na kula chakula chini ya mti Kajiado.
Rais Uhuru ameripotiwa kufanya mambo kadhaa ambayo hayajawahi kufanywa na Marais wengine wa nchi hiyo likiwemo la kutembea Nairobi bila msafara ambapo hivi juzi kuna video ilitoka ikidaiwa kumuonyesha Rais huyo akinunua karanga kutoka kwa watoto barabarani Nairobi.Hii picha ya leo hapo juu inadaiwa ni msafara wake uliosimama na kula chakula wakati akitokea Arusha Tanzania kwenye mkutano ambapo alitumia usafiri wa gharama nafuu (gari) na kuendeshwa kutoka Nairobi, siku kadhaa tu baada ya nchi hiyo kutangaza kuvunja safari za nje ya nchi za viongozi wa serikali zisizo za lazima ili kuokoa matumizi makubwa ya fedha.
Ni siku kadhaa pia baada ya Rais huyu kutangaza maamuzi ya kupunguza mshahara wake, naibu wake, Mawaziri na hata wakuu wa mashirika ya umma nchini humo.
Tazama jinsi fundi alivyookolewa dakika za mwisho kwenye jengo lililowaka moto
Ni moto ambao umetokea kwenye gorofa ya tano ya jengo moja huko Houston Texas Marekani ambapo kikosi cha zimamoto kilifanya pia jitihada za kumuokoa fundi ujenzi mmoja aliekua kwenye gorofa hilo dakika za mwisho wakati moto umeshashika.
Kuna njama kuvuruga Bunge
a “Uvumilivu una mwisho wake, ukifika wakati huo tutawaambia Watanzania
nini kinachoendelea na sisi tunakusudia kufanya kitu gani.
Dodoma/Dar. Kuna njama. Maneno haya mawili
ndiyo yametumiwa na pande mbili zinazopingana ndani ya Bunge Maalumu la
Katiba, kuelezea hali iliyojitokeza jana wakati wa kikao cha Bunge hilo
kuhusu mvutano wa mabadiliko ya kanuni.
Njama zinazoelezwa na pande hizo ni za kuvuruga
mchakato wa Katiba Mpya, zikirejea yaliyotokea jana jioni ikiwamo
zomeazomea hali iliyomlazimu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba,
Samuel Sitta kuliahirisha Bunge hadi leo jioni.
Baada ya kuahirisha Bunge hilo, Sitta alikutana na
waandishi wa habari na kusema kwamba kuna njama za baadhi ya wanasiasa
kutumia vurugu kuhujumu mchakato wa upatikanaji wa Katiba, badala ya
kujenga hoja.
Bila kuwataja wanasiasa hao, Sitta alisema ikiwa hawataki kuendelea na mchakato huo, basi waondoke na kuwaacha wenye nia njema.
“Wanasiasa hawa wamedhamiria kuvuruga mchakato wa
Katiba, tuhuma ambazo tumetuhumiwa leo na Lissu (Tundu) ni uongo na
uzushi, mimi sihusiki na kupeleka marekebisho ya kanuni kwenye Kamati ya
Kanuni na Haki za Bunge,” alisema Sitta.
Sitta alikuwa anajibu mchango wa mjumbe wa Bunge,
Tundu Lissu alioutoa mapema kwenye kikao cha jioni, akipinga
kilichoelezwa ni njama za kutaka kubadili kanuni kinyemela ili kumsaidia
mwenyekiti kulidhibiti Bunge.
Sitta alisema kwa kuzingatia kanuni ya 59 (1),
Kamati ya Uongozi ina mamlaka ya kupeleka marekebisho ya kanuni ili
kuliwezesha Bunge kufanya kazi vizuri.
Alisema hoja kwamba haiwezekani kufanyika
mabadiliko hata kabla ya kuanza kutumika kanuni, siyo ya msingi kwani
kila kitu kinabadilika kutokana na mazingira yake.
“Kamati ya Uongozi ndiyo ilipeleka waraka wa
mabadiliko ya kanuni kwa Kamati ya Kanuni na Haki kwa kuzingatia kanuni,
lakini hata kabla ya kujadiliwa na kamati husika inaonekana kuna
wajumbe ndiyo wameichukua na kuifikisha bungeni,” alisema Sitta.
Alisema kwa kiasi kikubwa marekebisho ambayo
yangesomwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Pandu Ameir Kificho, yalilenga
kutoa ufumbuzi wa kanuni ya 37 na 38 juu ya upigaji kura ama uwe wa wazi
au siri.
Sitta alisema pamoja na hilo, kulikuwa na
marekebisho ya msingi kama kuweka utaratibu mzuri wa majadiliano katika
kamati pia kuweka utaratibu wa vikao vya Bunge kuanzia Jumatatu hadi
Jumapili.
“Mengi ambayo alikuwa anayasema Lissu kama ni takataka hayakuwapo katika taarifa ya Kificho,” alisema Sitta.
Rais akistaafu afutiwe kinga’
Dar es Salaam. Wakati Bunge la Katiba likiwa
bado halijaanza kujadili Rasimu ya Katiba, taasisi moja ya viongozi wa
dini imetoa maoni mapya ikitaka Rais wa nchi awe tu na kinga anapokuwa
madarakani, akiondoka awajibike kwa matendo yake.
Mapendekezo hayo yalitolewa Dar es Salaam jana na
Baraza la Wadhamini la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT),
lilipokutana kwa ajili ya kutafakari kwa pamoja juu ya mchakato wa
Katiba Mpya.
Mkutano wa Baraza hilo linalojumuisha Askofu
Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Titus Mdoe,
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Musa Salum na Padri John Solomon,
uliongozwa na kaulimbiu ya ‘Katiba Moja Kwa Watanzania Wote, Pamoja
Tutafika’.
Mwenyekiti wa IRCPT, Jaji Mstaafu Raymond Mwaikasu
alisema tafakari inahitajika kuhusu kinga ya Rais na kwamba wao
wanapendekeza awe nayo anapokuwa madarakani, lakini kinga hiyo iondolewe
anapoachia madaraka, ili awajibishwe pale alipokosea.
Jaji Mwaikasu alisema pamoja na kwamba
waliwasilisha maoni kwa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, hatua ya
sasa inawalenga watu wenye lengo la kuingia Ikulu wakiwa na mawazo ya
kujinufaisha wao, ndugu, jamaa na marafiki zao badala ya kuwatumikia
wananchi.
“Hili linapaswa kutazamwa kwenye Katiba yetu mpya
na sisi hatutakuwa wa kwanza kufanya hivyo, ila itasaidia kuwafanya
viongozi kufuata maadili na iwapo itatokea Rais kuvunja Katiba, apelekwe
mahakamani na akikutwa na hatia, awajibike hata kwa kujiuzulu,” alisema
Jaji Mwaikasu. Naye Sheikh Salum alisema mali zote ni miliki ya Mungu,
hivyo zinapaswa kugawanywa kwa usawa na ikitokea mtu akajimilikisha ni
jambo lisilokubalika, hivyo ziwepo sheria za kuwabana viongozi wa aina
hiyo.
Askofu Mdoe alisema Rasimu ya Katiba ni nzuri
ingawa hakuna kitu kinachokamilika kwa asilimia 100, hivyo mazuri
yaboreshwe, upungufu usahihishwe na yaliyokosekana yapatiwe fursa.
Alisema malumbano yanayoendelea kwenye Bunge la
Katiba hayana tija kwani yana mwelekeo wa masilahi ya kisiasa badala ya
masilahi ya umma.
“Wamebadilisha hali waliyotakiwa kuwa nayo,
wanarudi katika makundi hasa ya kisiasa na mijadala kuwa ya kichama
zaidi, wakifika bungeni wawe wazalendo wajadili na kuacha ushabiki,”
alisema Askofu Mdoe.
Muundo wa Muungano
Kuhusu mjadala wa serikali mbili au tatu, Jaji
Mwaikasu alisema hauna tija isipokuwa jambo muhimu ni kujenga msingi
imara wa kuheshimiwa kwa Katiba itakayopitishwa. “Tunaambiwa Katiba
imevunjwa, tunafanya nini? muhimu ni kuangalia viongozi wanaohusika
wanadhibitiwa vipi, vinginevyo itakuwa ni bure,” alisema.
Alibainisha kuwa tatizo Bunge la Jamhuri ya
Muungano limelala na walioteuliwa kutetea wanatetea mikate yao, hivyo
akapendekeza kuwapo haja ya wananchi nao kupewa meno ya kuhakikisha
Katiba inalindwa, ili pale itakapothibitika Rais amevunja Katiba
wachukue hatua.
Seif: Hatuko tayari kujadili serikali mbili
Zanzibar. Makamu wa Kwanza wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama chake cha CUF
hakiko tayari kujadili mfumo wa Muungano wa serikali mbili kama
inavyotetewa na wabunge wa CCM na Rais Jakaya Kikwete.
Amesema tayari amewaandikia barua Rais Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kuwaeleza juu ya msimamo huo.
Maalim Seif alitoa msimamo huo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti mjini Unguja.
Isitoshe, alisema CUF imebaini kuwa kuna njama za
kufuta kipengele katika Katiba ya Zanzibar kinachosema; “Zanzibar ni
nchi” na kwamba hiyo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu kwa kuwa
Wazanzibari kamwe hawatakubali kufanya hivyo.
Maalim Seif alisema haikuwa mwafaka kwa Rais
Kikwete kukosoa mapendekezo ya Rasimu ya Katiba yanayotaka mfumo wa
Muungano kuwa wa serikali tatu.
Alisema Jaji Warioba aliweka kando itikadi yake ya
CCM katika utendaji wake kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuja na
uamuzi huo kwa vile ndiyo tiba ya kero za Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.
“Mapendekezo yaliyowasilishwa na Jaji Warioba
hayakuwa maoni yake, yale ni maoni ya wananchi, Tanganyika imevaa koti
la Muungano, ametoa ushahidi wake ili kujenga mwafaka katika kuendeleza
Muungano wenye mfumo wa serikali tatu,” alisema Maalim Seif.
Alisema Muungano wa serikali mbili hauvumiliki na
kama kuna watu wanaendelea kuutetea mfumo huo, Zanzibar inaweza kutumia
sheria yake ya kura ya maoni kuwauliza wananchi wanaotaka na wasiotaka
jambo hilo.
“Nimemwandikia barua Rais Kikwete, nakala
nimempelekea Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, Tanzania Bara
wanataka Zanzibar iondoe kifungu cha Katiba kinachosema Zanzibar ni
nchi, jambo hilo halitapita...tutafanya kampeni wananchi walikatae,”
alieleza Katibu Mkuu huyo wa CUF.
Alisema ni jambo la kusikitisha katika hotuba yake
alijisahau kama ni mkuu wa nchi na analihutubia Bunge Maalumu badala
yake akaegemea kuwa mwenyekiti wa CCM.
Alisema haikuwa sahihi kutoa vitisho na kutaja
ikiwa Serikali ya Muungano chini ya Serikali tatu italegalega, jeshi
litachukua madaraka ya nchi.
“Rafiki na ndugu yangu Kikwete, usifikiri huu ni
wakati ule wa Julius Nyerere, akisema yeye hakuna wa kumpinga. Mambo
yamebadilika, usijifanye ni Nyerere mpya, hakuna atakayekusikiliza na
kubabaika,” alisisitiza Maalim Seif.
Rwanda na A.Kusini kusuluhisha mgogoro
Rais Jacob Zuma wa Afrika-Kusini na Paul Kagame wa Rwanda wamekubaliana mjini Luanda Angola, kuanzisha mazungumzo ya pamoja ya kumaliza mzozo wao wa kidiplomasia
Jaribio la kumuua Kayumba Nyamwasa lilitibuka Afrika Kusini
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulianza kuzorota pale Rwanda
ilipowafukuza maafisa sita wa ubalozi wa Afrika Kusini, saa chache baada
ya Afrika Kusini kuwatimua wanadiplomasia watatu wa Rwanda kuondoka
nchini humo karibu wiki tatu zilizopita.Lakini Serikali ya Rwanda ilisema hatua ya kuwatimua maafisa sita wa ubalozi wa Afrika Kusini mjini Kigali ni ya haki na ilizingatia uchokozi ambao ulianzishwa na serikali ya Afrika Kusini yenyewe kwa kufukuza maafisa watatu wa ubalozi wa Rwanda.
Rwanda ilisema kuwa Afrika Kusini ndio ilianza uchokozi kwa kuwatimua mabalozi wake watatu
Nyumba yake iliharibiwa huku komputa na baadhi ya nyaraka zilichukuliwa.
Mkutano wa usalama uliofanyika mjini Luanda ulijadili hali kati ya nchi hizo mbili huku viongozi hao wawili wakikikutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu mzozo huo kutokea.
Rais Zuma alisema kuwa wamekubaliana kusuluhisha mgogoro huo na pia kupata taarifa ya pamoja ili kuweza kusuluhisha tofauti kati yao.
Kadhalika Rais Zuma aliongeza kwamba serikali yake inatekeleza wajibu wake wa kimataifa kwa kuwapa hifadhi watu wanaoomba. Viongozi hao wawili wamekubaliana kukutana kwa ajili ya kuzungumzia swala hilo baadaye.
Obama kukutana na Papa Francis
Obama Kukutana na Papa Francis
Rais Barrack Obama wa Marekani anatarajiwa kukutana na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, katika makao yake makuu huko Vatican.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Obama kukutana na papa Francis.Wawili hao wanatarajiwa kujadili namna ya kupunguza tofauti iliyopo kati yao katika maswala mengi mbali na kujaribu kuinua maisha ya watu maskini duniani baada ya takwimu kuonyesha kuwa tofauti ya mapato kati ya matajiri na Masiki inaendelea kupanuka .
Aidha viongozi hao wawili wanatazamiwa kujadili hali ilivyo Nchini Ukraine, na swala la upatikanaji wa amani mashariki ya kati.
Mwafaka baina ya mitazamo tata kuhusiana na maswala ya uavyaji mimba, matumizi ya dawa za kupanga uzazi na ndoa ya jinsia moja pia inatarajiwa kuwa kati ya mada itakayojadiliwa .
Mkuu wa Jeshi kugombea Urais Misri
Mkuu wa majeshi na waziri wa ulinzi Misri, Abdul Fattah al-Sisi, ametangaza kujiuzulu jeshini ili kugombea katika uchaguzi wa urais mwezi ujao.Wagombea wote wanapaswa kuwa raia.
Al Sisi alitazamiwa kujiuzulu na anatarajiwa kushinda kwa ukubwa
Ni Bayana kwana Sisi hatakua na kibarua kigumu kujipatia ushindi katika uchaguzi wa Urais. Anaungwa mkono na idadi kubwa ya raia wa Misri na hadi sasa hana wapinzani wowote.
Baadhi ya waliotaka kugombea urais wamejiondoa wakidai kwamba hawataweza kuendesha kampeni zao kwa njia huru.
Wafuasi wake Sisi wanamuona kama kiongozi imara ambaye anaweza kurejesha amani na udhabiti nchini Misri baada ya miaka mingi ya machafuko.
Wakosoaji wake wanasema ana msimamo mkali na amechangia pakubwa katika kusambaratisha na kuhujumu upinzani nchini Misri.
Mkuu huyo wa jeshi atakabiliwa na majukumu mazito ya kufufua uchumi uliofifia , kupambana na uasi na kuileta pamoja nchi iliyogawanyika. Ameahidi kutekeleza mabadiliko makubwa lakini akaonya kuwa hawezi kufanya miujiza.
Subscribe to:
Posts (Atom)