Tuesday, 11 March 2014
Abiria wanaotumia kituo cha gereji barabara ya mandela kwa siku mbili mfululizo wamekuwa wakipata kero ya harufu kali inayosababishwa na gari ya kubebea taka iliyopaki kwenye kituo hiko.Wakiongea na mtandao wa wetu huu wa Dj sek abiria hao wamesema kwamba gari hiyo iliharibika ikiwa inaelekea kumwaga uchafu huo na wakaisogeza kituoni hapo ili waweze kuitengeneza, lakini badala yake dereva na wasaidizi wake wakaitelekeza gari iyo toka juzi.Wakiendeleaa kuongea na mtandao wetu wamesema eneo lote la kituoni hapo linatoa harufu kali ambayo ni kero kwa wao wanaosubilia usafiri eneo hilo.
KAMPUNI YA GOOGLE YAKANUSHA PICHA YA GOOGLE MAP INAYOONESHA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA
KAMPUNI YA GOOGLE YAKANUSHA PICHA YA GOOGLE MAP INAYOONESHA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA
"Yes, the images may be there, but it is not real time satellite images as the images may have provided to us several weeks or months ago," he said when contacted.
Hii imetokana na kutapakaa kwa picha inayoonesha ndege ya Malaysia Airline imedondoka kwenye maji.
Mpaka sasa meli zipatazo 40 na ndege 34 zinazunguka bahari inayizunguka maeneo ya Vietnam na Malysia wakitafuta ndege ya Malaysia Airline iliyopotea toka jumamosi.
Nchi zinazoshiriki kuitafuta ndege hiyo ni Australia, China, Thailand, Indonesia, Singapore, Vietnam, Philippines, New Zealand na Marekani.
Askofu Mtetemela awatuliza wananchi
Dodoma. Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania,
Donald Mtetemela amewahakikishia Watanzania kuwa Katiba itapatikana kwa
wakati.
Hata hivyo, amesema kuna haja kwa Watanzania wa
dini zote kuliombea Bunge Maalumu la Katiba lifanye mambo kwa
kumshirikisha Mwenyezi Mungu ili mchakato wa Katiba uende vizuri.
Askofu Mtetemela, ambaye ni mmoja wa mjumbe wa Bunge hilo, alitoa ushauri huo jana kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Alisema kuyumba kwa Bunge la Katiba kwa sasa
kunatokana na misimamo ya vyama vya siasa na kwamba kitendo hicho
kimesababisha kuchelewa kwa kazi ya msingi.
“Mambo ya misimamo hayawezi kuzuilika na wala si
kosa kila kikundi kuwa na msimamo wake, lakini kinachotakiwa ni wajumbe
kufuta mambo ya vyama vichwani mwao na hasa pale panapokuwa na hoja ya
msingi,” alisema kiongozi huyo wa kiroho.
“Watanzania waendelee kutuombea kwa nguvu zote.
Sina shaka tutatoka hapa tukiwa wamoja kwa sababu tunaimba wimbo mmoja
wa kutaka kitu kizuri mbele yetu,” alisisitiza Askofu Mtetemela.
Askofu Mtetemela alisema kuwa katika hatua za
awali kulikuwa na misukosuko mikubwa ndani ya Bunge, lakini sasa kuna
mwelekeo wa kuridhisha kutokana na wajumbe kuelewa wajibu wao katika
mchakato huu.
Bunge Maalumu la Katiba sasa vululu vululu
Dodoma. Matarajio ya Bunge Maalumu la Katiba
kukamilisha kanuni kwa maridhiano yaliyeyuka tena jana huku mambo ndani
ya ukumbi yakionekana kuwa vululuvululu kwa baadhi ya wajumbe kuzungumza
nje ya utaratibu na wengine kurushiana vijembe.
Baadhi ya wajumbe waliamua kutoleana lugha chafu
na kuweka kando hoja za msingi zinazowafanya watofautiane na
kuchelewesha kazi ya kuandika Katiba Mpya.
Hali ilichafuka mchana wakati wajumbe walipokutana
kupitisha kanuni baada ya mmoja wao, Felix Mkosamali kuomba mwongozo
kwa Mwenyekiti wa muda, Pandu Ameir Kificho. Hata hivyo, Kificho
alimtaka kukaa chini kwa muda kwa maelezo kuwa wajumbe waliofika katika
kikao hicho walikuwa wachache, hivyo mwongozo wake kama ulikuwa
unahitaji majibu ingekuwa vigumu kutolewa.
Baada ya muda alisimama, James Mbatia na kuomba
mwongozo, akihoji sababu za kutaka kuanza kikao cha kupitisha kanuni
hizo wakati wajumbe hawajapewa vitabu vya rasimu ya kanuni zenyewe.
“Mwenyekiti ulitangaza asubuhi kuwa tutagawiwa
kanuni kabla ya saa tisa lakini hadi sasa tunataka kusomewa kanuni
wakati hatujagawiwa kanuni hizo,” alihoji Mbatia.
Kificho alitoa ufafanuzi kuwa kanuni hizo zilikuwa
bado zinadurufiwa na kuwataka wajumbe wawe na nidhamu kwani
anapotangaza wanapiga kelele.
Ghafla alisimama Mkosamali tena na kuwasha kipaza
sauti na kuhoji kitendo cha mwenyekiti huyo kumpa Mbatia nafasi ya kutoa
mwongozo wakati yeye amenyimwa... “Mwenyekiti hivi unaongozaje kikao,
inakuwaje mimi nikuombe mwongozo uninyime na mwenzangu umpe? Mwenyekiti
nakuheshimu sana, lakini sijui unatumia kanuni ipi kutoa nafasi kwa
mjumbe wakati mimi ulinizuia nisiseme,” alihoji Mkosamali.
Baada ya kauli hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Hawa Ghasia aliwasha kipaza sauti na kwa sauti ya juu
alisema “Mtoto mdogo hana adabu.” Kauli hiyo iliibua hasira za Mjumbe
mwingine, Moses Machali ambaye naye aliwasha kipaza sauti na kumjibu:
“Kubwa jinga halina adabu,” kauli iliyoibua miguno ndani ya Bunge.
Hata hivyo, licha ya Mwenyekiti kutoa onyo kwa
kauli hizo kwamba hazifai, Mkosamali alisimama katika sehemu yake na
kusema kuwa hakuna mtoto mdogo na kwamba tangu lini mtoto aliishinda
CCM.
Chanzo cha tatizo
Chanzo cha mvurugano huo ambao wiki iliyopita
kidogo usababishe ngumi kurushwa bungeni, ni mfumo wa upigaji kura
katika kupitisha ibara za rasimu, ambao jana uliendelea kuwagawa wajumbe
na kufanya ukumbi huo kuonekana kama eneo la mzaha.
Kauli za ‘ndiyoooo’, ‘hapanaaaa’ na vitendo vya
kugonga meza viliongezeka katika kipindi cha asubuhi baada ya Mwenyekiti
wa Kamati ya Kuandaa Kanuni, Profesa Costa Mahalu kuwaleza wajumbe kuwa
kamati yake haijafikia mwafaka wa ama iwe kura za siri au wazi na
kwamba suala hilo limerejeshwa kwa wajumbe wenyewe.
Meli ya Korea Kaskazini yanaswa Libya
Wakuu nchini Libya, wamesema kuwa wameikamata meli moja iliyokuwa na bendera ya Korea Kaskazini, ikiwa na shehena haramu ya mafuta katika bandari inayodhibitiwa na waasi.
Maafisa wa serikali ya Libya waliisimamisha Meli hiyo ya Korea Kaskazini ilipokuwa ikiondoka kutoka bandari inayodhibitiwa na waasi siku ya Jumatatu ikiwa imesheheni mzigo usio rasmi wa mafuta ghafi.
Jeshi la nchi hiyo limethibitisha tukio hilo.
Waasi wa zamani wanaotaka kuitenga eneo la Libya Mashariki, wamekuwa wakimiliki bandari ya Al-Sidra na vituo vingine muhimu vya kuuzia bidhaa nje katika eneo hilo tangu Julai mwaka uliopita.
Mnamo siku ya Jumamosi, walianza kupakia shehena ya mafuta yasiyosafishwa ndani ya meli hiyo ya Korea Kaskazini iitwayo Morning Glory, iliyokuwa imetia nanga katika bandari ya Al-Sidra.
Viongozi walaani wizi wa mafuta
Kiwanda cha mafuta nchini Libya
Chama kikuu cha kisiasa nchini humo cha General National Congress, GNC, kimethibitisha kuzuiliwa kwa meli hiyo.
Runinga ya taifa Nchini Libya Al-Nabaa pia imeripoti tukio hilo kwa undani.
Walid al-Tarhuni, ambaye ni msemaji wa zamani wa kundi la waasi ambalo limekuwa likidhibiti bandari hiyo, ameiambia runinga ya Al-Nabaa kuwa meli hiyo ya mizigo ilikuwa ikielekea katika bandari ya Zawiyah, kilomita 50, Magharibi mwa mji mkuu Tripoli, kupakua mafuta hayo.
Utawala wa Washington umesema kuwa umeshangazwa na tukio hilo na kukariri kuwa mafuta inayotoka Libya ni mali ya raia wa nchi hiyo na wala sio ya makundi fulani.
Malaysia yazidisha kasi kutafuta Ndege
Zoezi la kutafuta ndege ya abiria ya Malaysia limeendelea kushika kasi baada ya kuwepo kwa hali ya sintofahamu na wasiwasi mwingi kutoka kwa ndugu za watu waliopotea wakiwa katika ndege hiyo.
Ndugu wa waliopotea wameelezwa kuwa wakae tayari kupata habari mbaya
Mamlaka nchini Malaysia zinasema wameongeza mipaka ya eneo la utafutaji, mara mbili Zaidi, huku China ikiwa imepeleka mitambo 10 ya satelaiti kwa ajili ya kusaidia kutafuta ndege hiyo.
Mkuu wa Idara ya anga Azharuddin AbdulRahman amewaambia waandishi wa habari kuwa eneo la kusaka ndege hiyo limeongezeka mara mbili kutoka maili 50 za baharini kunakosemekana ndege ilipotelea mpaka maili 100.Ndege iliyokua imebeba watu 239 ilipotea bila kutoa taarifa yeyote na hakuna dalili yeyote mpaka sasa ya kupatikana kwa mabaki ya ndege hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)