Thursday 20 February 2014

MSANII BONGO MUVI ANASA KWENYE MTEGO WA KUJIUZA

MSANII BONGO MUVI ANASA KWENYE MTEGO WA KUJIUZA

ILE skendo ya kukithiri kwa baadhi ya mastaa Bongo kujiuza imechukua sura mpya kufuatia msanii wa Bongo Movies, Isabella Francis ‘Vai wa Ukweli’ naye kunasa mtegoni, Ijumaa lina kisa kizima.

Vai wa Ukweli akiwa mawindoni.

Tukio hilo la aibu kwa tasnia ya sinema nchini lilijiri usiku wa kuamkia Jumanne iliyopita, Sinza ya Vatican jijini Dar es Salaam ambapo baada ya kuumbuka, Vai alijikuta akiangua kilio na kuomba siri hiyo isisambae.
VAI WA UKWELI NI NANI?
Vai ni msanii wa filamu za Kibongo kwa muda mrefu. Amecheza filamu kadhaa zikiwemo Beautiful Liar (ya kwake mwenyewe), Family Apart, Good Fellow na nyinginezo.

 
Vai wa Ukweli akificha uso wake baada ya kunaswa.
MALALAMIKO KWA OFM
Ikiwa katika kutega ‘rada’ zake, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilipokea malalamiko ya listi ya wasanii wa kike wa Bongo Muvi wakidaiwa kujishughulisha na uuzaji wa miili huku jina la Vai likiwa miongoni mwao.
  

MCHEZO WAANZA
Kilichofanyika, Vai aliwekewa mtego na kujikuta akiingia mzimamzima. Fuatilia uhondo wa mawasiliano kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS, tunazo):
OFM: Mambo Vai? Naitwa Salum, natokea Arusha ila kwa sasa nipo Dar, naomba kuonana na wewe.
Vai: Ili?

OFM: Kusema kweli nimetokea kukupenda, nimetafuta namba yako nikaipata nikaona nikutafute.
Vai: Muda sina.

OFM: Please usiniangushe, nitakupa chochote utakacho, nakuomba.
Vai: Nani kakupa namba yangu?

OFM: Sijakuelewa.
Vai: Umetumwa wewe, siyo bure.
OFM: Hivi mtu unaweza kutumwa kumpenda mtu jamani? Usinifanyie hivyo, nipe hiyo nafasi Vai, utafurahia.

ANAINGIA, ANATOKA
Vai: Oke, kwa nafasi umechelewa maana boy ninaye. Kwani umefikia wapi?
OFM: (OFM yamdanganya) niko hoteli moja inaitwa Lunch Time hapa Tip Top Manzese (Dar), wewe uko wapi?

Vai: Mwananyamala (Dar), njoo nikuone.
OFM: Nimekuja huku Kariakoo kufungasha mzigo, we huwezi kuja pale hotelini baadaye? We si ni mwenyeji sana Dar?
Vai: Siwezi.

OFM: Sa tunafanyaje wangu? Nitaumia sana kama nitaondoka bila kukuona, nakupenda.
Vai: Ndo hivyo ukiweza njoo Mwananyamala.
OFM: Huko mimi ni mgeni wangu, nitalipia gharama zako, usininyong’onyeshe.
Vai: Tuma hela ya Bajaj kwa …(unatajwa mtandao) nitakuja.
OFM: Sawa nitakutumia, ni shilingi ngapi kutoka huko hadi hapa hotelini?
Vai: Kumi na tano tuma.

OFM: Sawa na ofa yako tukionana ni shilingi ngapi?
Vai: Ofa ya nini?
OFM: Si tukionana jamani ili nijiandae nisije nikaumbuka, unajua tena watu kama nyie…
Vai: We sikuelewi kwani kuna nini tofauti, kuonana umetaka nimekubali bado unaongea tofauti.
OFM: Tofauti vipi jamani?
Vai: Unazingua.

OFM: Nazingua vipi?
Vai: Tuma hiyo hela nije.
OFM: Pesa ya kujia siyo ishu, natuma twenty (20,000), nataka kujua shilingi ngapi utataka kuwa na mimi kwa leo ili nijiandae wangu, naomba uelewe.
Vai: Tutaongea usijali.

OFM: Kwa hiyo wangu, niambie basi.
Vai: Usijali nikija tutaongea.
OFM: Nataka ukija nisisumbuke, we niambie tu unataka shilingi ngapi kwa kuwa na wewe leo, nataka nikachukue pesa ATM, we mtu mzima bwana!

Vai: Oke siwezi, achana na mie. By the way mimi sijiuzi.
OFM: Siyo suala la kujiuza Vai, kama unataka nikukose sawa lakini ningefurahi sana, kuwa nawe, acha pesa, nitakupa utakachotaka.
Vai: Siwezi.
OFM: Usinifanyie hivyo utaniumiza.

Vai: Si nimekuambia tuma nauli nije? Tutaongea hujiamini.
OFM: Ujue nakuuliza hivyo ili nijipange hata kama ni kuchukua pesa nichukue za kutosha kwa leo.
Vai: Kama huelewi basi.
OFM: Kama sielewi nini? We niambe tu.
Vai: Milioni.

OFM: Milioni moja?
Vai: Ndiyo.
OFM: Usikomae Vai, nimetumia pesa nyingi kufungashia mzigo, nifanyie fea wangu. Hiyo m moja tutalala?
Vai: Siwezi.
OFM: Huwezi kulala? Sikia, nifanyie laki tano basi, ila itakuwa poa kama tutalala maana mshikaji niliyekuja naye kaondoka leo.

Vai: Kulala siwezi.
OFM: Kwa mfano kuanzia saa moja mpaka saa ngapi hivi naweza kuwa na wewe? Labda nikuambie ukweli, kwa nini nimekutafuta, kuna picha yako niliichukua kwenye gazeti  nikakupenda sana, nikawa namaliza shida zangu, nimekuja Dar ndo nikasema nikutafute unipe live kwa gharama yoyote Vai.
Vai: Kimya.

OFM: Subiri kidogo wangu nakutumia.
Vai: Mh! Kwa nini muda unaenda, kama umebanwa basi siku nyingine.
OFM: Noo please kuna mtu nimemwambia akutumie 15 (15,000/=) sasa hivi wangu, mambo mengine ukija, ukiipata niambie, sawa ee..
Vai: Mh!
OFM: Nini jamani tena?

BAADA YA DAKIKA NANE
Vai: Oke nimekuelewa. Nimeipata
OFM: So unatoka huko saa ngapi? Kwani ni mbali?
Vai: Ndiyo, wewe uko wapi?
Vai: Nikija sitaki uswahili, mie naogopa magazeti, sawa kaka, sasa unanipa changu nafanya kazi yako.
Vai: Nipigie.
Vai: Uko kwa wapi maana mimi nipo Vatican (Sinza, Dar).

KABANG!
Baada ya kuchati kwa muda mrefu bila kujua anaingia mtegoni, hatimaye Vai alifika kwenye Kituo cha Daladala Vatican lakini hakutaka kushuka kwenye Bajaj.
Badala yake alimtaka kachero wetu ambaye ni Salum wa bandia kuingia kwenye usafiri huo kisha akamuongoza dereva kuelekea Baa ya Mawela iliyopo jirani na eneo hilo.
Akiwa amejiaminisha kuwa analamba laki tano yake, Vai alianza kuagiza pombe za bei mbaya huku akisisitiza kupewa chake kwanza ili akampe huduma.

HALI YABADILIKA GHAFLA
Hata hivyo, hali ilibadilika ghafla, hebu fuatilia mazungumzo yao:
Vai: Vipi mbona kama hujiamini? Kabidhi laki tano yangu kieleweke.
Kachero wa OFM: Vai sikiliza, mimi si pedeshee wala mfanyabiashara wa Arusha. Ni kachero wa OFM (Oparesheni Fichua Maovu) ya Global Publishers. Tunafichua uovu ndani ya jamii.
Vai: (huku akihamaki) kaka hebu nioneshe ‘toileti’ zipo wapi hapa?

Kachero wa OFM: Toileti zile pale.
Vai alikwenda toileti ambako alikaa huko takriban dakika tatu. Cha ajabu, alirejea akiwa analia ambapo mambo yalikuwa hivi:
Vai: Unasema wewe ni mwandishi wa Global? Si kweli, nawajua wote ila wewe siyo!
Kachero wa OFM: Unatakiwa kusadiki haya niyasemayo.

Vai: Kama kweli nioneshe kitambulisho.
Kachero wa OFM: (huku akikitoa) hiki hapa.
Vai: Hamna. Kama ni kweli niitie Sifael (Paul) na Erick (Evarist) waje hapa.
Kachero wa OFM: Hakuna shida Vai, twende ofisini Bamaga-Mwenge wamejaa tele usiku huu.

Baada ya kusikia hivyo, Vai alinyanyuka na kwenda eneo la kuegesha magari na kuzua tafrani, ndipo kijana mwingine wa OFM aliyekuwa akilinda usalama wa mwenzake akatoa vifaa vyake vya kunasia matukio ambapo alimrekodi Vai akizua timbwili bila kujua.
Mbele kidogo ya baa hiyo, Vai aliita Bajaj na kumwagiza dereva amkimbize Global Publishers.
Alifika kwenye ofisi za gazeti hili akiwa anahema mithili ya mbogo aliyejeruhiwa ambapo alitulizwa na wahariri waliokuwa mzigoni na kufanya mahojiano:

USO KWA USO NA WAHARIRI
Wahariri: (wakijifanya hawaelewi chochote) nini kimetokea Vai?
Vai: Ninyi mnajua kila kitu. Kwa nini mmeniwekea mtego? Kuna jamaa anadai ni mwandishi wenu, alijifanya mfanyabiashara akawa anawasiliana na mimi.
Wahariri: Mlikuwa mnawasiliana kuhusu nini?
Vai: Alisema sijui aliniona kwenye gazeti akanipenda, amekuja Dar akaamua kunitafuta.
Wahariri: Kukutafuta kwa nini?

Vai: Alitaka akalale na mimi kwa laki tano.
Vai: Tulikubaliana tukutane lakini mimi sikuwa na mpango wa kwenda kulala naye. Nilitaka nichukue hiyo laki tano yake nimpe sababu za ‘kiwanawake’ so nisingefanya naye ngono.

Wahariri: Ina maana huwa unafanya hivyo? Huoni hatari kuchukua fedha ya mtu na kuingia mitini? Huo si ni utapeli? Huogopi kutafutwa na kufanyiwa kitu mbaya?
Vai: Naamini angenielewa tu (kilio mfululizo).

STEVE NYERERE, MTITU
Baada ya Vai kukiri kuingia kwenye mtego wa kujiuza, gazeti hili liliwasiliana na baadhi ya viongozi wao kuwasikia wanalizungumziaje tukio hilo.
Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity alisema: “Tunawafukuza wote mnaowanasa, hawana sifa ya usanii, wanaingia kutimiza ndoto zao za kujiuza. Hawafai Bongo Muvi.”

Naye Katibu wa Bongo Movie Unity, Wiliam Mtitu alifunguka: “Tutakaa kikao tumfukuze Bongo Muvi, ametuchafua sana.”
Mmoja wa mastaa ambaye hakutaka kutajwa jina alidai kuwa umefika wakati kwa mastaa kujilinda wakitajwa warembo kama Wema Sepetu, Jokate Mwegelo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Aunt Ezekiel, Jacqueline Wolper na wengine kwamba siku wakinaswa itakuwa ni aibu kubwa.

WENGINE KWENYE ‘TAGETI’
Listi ya mastaa wanaojiuza kwa mapedeshee iliyopo mikononi mwa OFM ni ndefu, kikosi bado kiko mzigoni kuwanasa.

KAZI NZURI YA OFM
Tangu OFM imeanza kazi yake nzuri ya kufichua maovu, kabla ya Vai tayari ilishawanasa mastaa watatu wa Bongo Muvi, Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ na Baby Joseph Madaha.


 

KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI AWASILI MKOANI RUKWA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU, AAHIDI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA VITEULE VYA JESHI VYA KIRANDO NA KASANGA MKOANI RUKWA 

 

Katibu Mkuu wa Wiazara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Ndugu Job Masima akishuka kwenye ndege aina ya Auric Air katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga mapema jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Rukwa kufuatia mwaliko wa Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella 
Manyanya.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kulia akimtambulisha Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Symthies Pangisa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga jana.
 
Katibu Mkuu wa Wiazara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akisalimiana na mwanasiasa Mkongwe nchini Ndugu Chrissant Mzindakaya katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. 

ANGALIA KAULI YA ZITTO KABWE KUHUSU NYONGEZA YA POSHO BUNGE LA KATIBA





zito  



Ishu ya posho za bunge la katiba ndiyo inayoongelewa sana hivi sasa ambapo pamoja na headlines zote za Wabunge, haya ni mawazo ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuhusu hii posho.
 
 Screen Shot 2014-02-20 at 11.43.10 AM

MAKAMU WA CCM BARA MH.PHILIP MANGULA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO BEIJING CHINA

 

Makamu wa ccm bara MH.Philip Mangula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watanzania wanaosoma na kufanya kazi nchini China katika mji wa Beijing baada ya kukutana nao kwa kikao kifupi katika kujadili mstakabali wa wasomi katika ujenzi wa taifa lao.Hii ilifanyika baada ya ziara fupi nchini aliyofanya MH,Mangula mwanzoni wa wiki hii.

 

WAWILI WAONDOLEWA BUNGE LA KATIBA: Baada ya kubainika wanatumia majina yanayofanana!

 

 Uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete wa wajumbe 201 wa Bunge Maalumu la Katiba, umekumbwa na dosari baada ya wajumbe wawili wenye majina na ubini unaofanana, Amina Mweta, kutinga bungeni kila mmoja akidai kuwa mjumbe halali.

Habari zilizopatikana jana mjini Dodoma zinasema wajumbe hao wanaotokea kundi la wafanyakazi, wamelipwa posho za awali lakini walizuiwa kuendelea na taratibu nyingine kusubiri hatima ya utata wa suala lao. 
Habari zilisema baada ya kuwasili bungeni, wajumbe hao walijisajili kwa nyakati tofauti na kila mmoja kupewa vitambulisho.Mmoja alipata chenye namba 602 na mwingine 1308.
  

Wajumbe hao walikiri kulipwa posho ya kujikimu ya Sh80,000 kwa siku kwa muda wa siku 13 unaomalizika Februari 28 mwaka huu ikiwa na maana kwamba kila mmoja alilipwa Sh1,040,000. 
Habari zilidai kuwa Amina Mweta wa kwanza anatoka katika Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) na mwingine anatoka katika Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Usafirishaji (COTWU). 
Mkanganyiko huo ulitokana na kuwapo kwa sehemu nyingi za usajili wa wajumbe hao kiasi kwamba watumishi wa Bunge walishindwa kubaini kuwapo kwa Amina Mweta wawili kutoka kundi moja.
Mmoja wa kina mama hao anatokea wilayani Mwanga, Kilimanjaro na mwingine Songea, mkoani Ruvuma. 
Mweta kutoka Mwanga alisema alipigiwa simu na Ofisi ya Bunge Maalumu la Katiba na kupongezwa kwa kuteuliwa na Rais kuwa mjumbe. 
“Mimi ni personal secretary (katibu muhtasi) wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga na nilipigiwa simu na Ofisi ya Bunge wiki iliyopita nikipongezwa kwa uteuzi huo,” alisema. 
Alisema alipofika na kujisajili baada ya kutoa kitambulisho chenye jina lake, alipewa kitambulisho na kisha kupewa malipo yake ya posho. Mweta kutoka Songea alisema alipigiwa simu na Katibu Mkuu wa COTWU kwamba ameteuliwa na Rais kuwa mjumbe na kutakiwa kuripoti bungeni. 
Kama ilivyokuwa kwa mwenzake wa kutoka Mwanga, alisema naye alijisajili na kulipwa posho ya siku 13 na jana alishangaa kukuta mjumbe mwingine mwenye jina kama lake. 
Alisema viongozi wa COTWU wamemwambia asubiri wakati wakitafuta usahihi wa nani hasa kati yao mwenye uhalali wa kuwapo bungeni. 

Ofisi ya Rais yatoa msimamo 
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alipoulizwa kuhusu mkanganyiko huo, alisema hajapata taarifa rasmi lakini watakapozipata watathibitisha nani aliyeteuliwa na Rais kuwa mjumbe wa bunge hilo. 
“Aliyeteuliwa na Rais ni mtu mmoja na ndiyo maana huwa tunapenda watu watumie majina matatu kwa sababu kwenye nchini kunaweza kuwa hata na watu 10 wote wanatumia jina moja. 
Tukipata taarifa rasmi tutakachofanya ni kuthibitisha nani haswa aliyeteuliwa na Rais ambaye ataendelea kuwa mjumbe na huyo mwingine basi itakuwa ni bahati mbaya,” alisema Balozi Sefue.
Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alipoulizwa kuhusu utata huo alisema mjumbe halali ni yule aliyetoka Songea. 
Hata hivyo, alisema kinachowashangaza ni kwama yule mwenzake wa Mwanga alipotakiwa kurudisha fedha alizopewa kimakosa alisema ameshatumia sehemu kubwa na kubakiza Sh50,000 tu. 
MWANANCHI

 

MCHAWI WA UNGO ADONDOKA, AGEUKA KUKU 

Stori: Joseph Ngilisho, Arusha
HALI ya taharuki iliyoambatana na imani za kishirikina iligubika Jiji  la  Arusha kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina kudondoka na ungo wa kishirikina asubuhi ya Ijumaa iliyopita kisha ghafla kubadilika  kuwa kuku mweupe mwenye mayai ndani ya ungo, Uwazi limeona mengi.

Mamia ya wananchi katika eneo la Kimandolu kando ya Barabara ya Arusha- Moshi walimiminika kushuhudia tukio hilo lililojiri saa tatu asubuhi.

Akizungumza na Uwazi, shuhuda mmoja wa tukio hilo ambaye ni dereva wa bodaboda, Martin Mbise alisema:
“Nilikuwa kwenye shughuli zangu za kila siku, ghafla niliona kitu kipana kikidondokea kwenye huu mtaro, ndani yake nikamwona mtu amekaa akiwa uchi wa mnyama.

“Wengi tuliamua kusogelea eneo la tukio, lakini kabla hatujakifika, mtu huyo alitoweka, badala yake mle mwenye ungo  mkawa na kuku mweupe na mayai zaidi ya kumi, tulishangaa sana:
Mbise alisema hali hiyo ilidumi kwa saa mbili na nusu, ndipo wananchi hao wakaamua kumchoma moto kuku huyo baada ya kumuua na kuyavunja mayai.

Hata hivyo, alisema haikuwa rahisi kuku huyo kuungua licha ya kumwagiwa mafuta ya taa na petroli na wakachukua uamuzi wa kumkatakata na kugawana nyama yake huku baadhi
yao wakikimbia hovyo na kulaani tukio hilo.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema tukio hilo ni laana na anapaswa kuitwa mtumishi wa Mungu kwa ajili ya kukemea pepo mchafu kwa maombi ya kiroho wakiamini mchawi huyo alikuwa ana lengo la kuwadhuru.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Lebaratus Sabas hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo, lakini baadhi ya maafande waliofika katika eneo hilo walithibitisha. 

NAPE "WANAOTAKA SEREKALI TATU NI WAHUNI"

Wanaotaka serikali tatu ni wahuni" Nape Nnauye:Hii kauli ya Katibu wa Itikadi na Uwenezi wa CCM,Nape kumtukana Mwenyekiti wa chama chake na Raisi wa nchi.

Tume inayongozwa na Jiji Warioba,iliteuliwa na Raisi hivyo kuwaita wanaotaka serekali tatu ni wahuni,afahamu kwamba kamtukana mkuu wake na sio mwingine.

Na kama raisi alipokea maoni rasimu iliyokuwa na serekali tatu,ambazo Nape anaita ni wahuni,sasa asilimia 63% ya watz ni wahuni?

JK hataki misimamo ya vyama bungeni, nyie serekali mbili mnatoa wapi?

Maoni ya watanzani yanatakiwa kuheshimiwa na kulindwa kwa gharama yoyote hata ikibidi,kumwajika kwa damu,Lengo kuheshimu Sauti ya Umma

AJABU:MWANAMKE ANAYE LIA NA KUTOA MACHOZI YA DAM

Miaka minne iliyopita msichana huyu mwenye umri wa miaka 19, Delfina Cedeno, alianza kupata tatizo hili la ajabu, lililokuwa likimfanya alie na kutoka jasho la damu. Kwa kuongeza zaidi, wakati mwengine damu zimekuwa zikitoka hata kwenye kucha na kitovu.

Hali hii ilipomuanza, alianza kwa kulia machozi mekundu, kutokwa na damu puani na kunyunyukwa nywele kichwani.

Hali ilipokuwa mbaya, alikuwa akienda hedhi kwa siku 15 mpaka ikafika kipindi alihitaji kuongezwa damu kutokana na hali hiyo iliyokuwa ngumu. Licha ya vipmo vingi alivyofanya, madaktari wa mji wake wa Veron, kwenye Jamhuri ya Dominica, walishindwa  kumsaidia.
Cedeno alisema: ‘Hali hii ilipoanza kwangu sikuwa najua nini cha kufikiri – nilishtushwa na kuogopa.
Anasema alijisikia vibaya kutokana na hali aliyokuwa nayo mpaka ikambidi aondoke nyumbani kwao alipokuwa akiishi na mama yake aitwaye Mariana, 36.
Aliacha shule huku marafiki zake wengi wakimtenga kutokana na hali hiyo wakihofu kupata maambukizo au usumbufu kutokana na hali yake.

‘Nilitengwa, ila Mungu mkubwa. Kwa sasa najisikia poa maana baada ya muda mrefu nimeanza kujisikia vizuri.’
Miezi michache baadae alifanikiwa kupata boyfriend, Recaris Avila, ambaye alimtembelea hospitali mara baada ya kusikia stori yake. 

 WATOTO WALIO ZALIWA WAMEUNGANA WAREJEA DAR BAADA YA KUTENGENISHWA

Watoto pacha, Elikana na Eliud waliokuwa wameungana wamerejea nchini jana wakitokea India walipokuwa kwa ajili ya kutenganishwa, tayari kwa kusherehekea kumbukumbu yao ya kutimiza mwaka mmoja leo.

Waliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa 10:30 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Oman, wakiwa na mama yao, Grace Joel (20) ambaye muda wote alionekana mwenye furaha.

Elikana na Eliud walizaliwa Februari 20, mwaka jana wilayani Kyela, Mbeya wakiwa wameungana na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambako walipata rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Juni mwaka jana, Serikali iliwapeleka Hospitali ya Chennai, India ambako Desemba 16, mwaka jana walifanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha.

Akizungumza baada ya kutua jana, Grace alisema: “Nina furaha ya ajabu, sijui nimshukuru vipi huyu Mungu wangu, ni mkuu mno. Ninawashukuru sana madaktari wa India, ninawashukuru madaktari wa Muhimbili na sana naishukuru Serikali yangu kwa kunipa msaada huu mkubwa. Siamini kama leo ningekuwa narudi salama na watoto wangu kila mmoja akijitegemea,” alisema Grace.

“Kesho (leo) ni birthday yao, wanatimiza mwaka mmoja, ni furaha ya ajabu niliyo nayo, siwezi kuelezea. Siku nilipoambiwa watoto wangu watafanyiwa upasuaji mkubwa na watapumulia mashine kwa wiki moja, nilichanganyikiwa kwa kweli, sikutamani tena hata hiyo operesheni ifanyike ila sikuwa na jinsi zaidi ya kumwomba Mungu.”

Akizungumza uwanjani hapo, Dk Glory Joseph kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando ambaye aliongozana na watoto hao kurudi nchini alisema: “Watoto wamerejea salama na wanaendelea vizuri ila watakuwa Moi (Hospitali ya Mifupa Muhimbili), kwa uangalizi maalumu mpaka hapo madaktari watakapoona inafaa ndipo watapewa ruhusu ya kurudi nyumbani kwao Mbeya.



MABASI YA MAJINI KUMALIZA MSONGAMANO WA MAGARI JIJINI DAR!!




 Serikali, mashirika binafsi na wadau wa usafiri ndani na nje ya nchi wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali kukabiliana na msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam. Msongamano huo ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na uduni wa miundombinu ikiwemo barabara, umekuwa ni kero kwa wananchi na Serikali kwa jumla. Serikali imewekeza katika Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (BRT) na usafiri wa treni ndani ya Jiji la Dar es Salaam kama njia mojawapo ya kumaliza tatizo la msongamano wa magari na foleni. Msingi wa tatizo Chanzo kikubwa cha foleni jijini Dar es Salaam si wingi wa abiria bali ni wingi wa magari binafsi na njia finyu zisizokidhi mahitaji ya watu walioko katika jiji hilo. Njia muhimu ya kupunguza foleni na msongamano wa magari ni kupunguza wingi wa magari barabarani na kuweza kuzipanua barabara ili kuwe na uwezekano wa kupita kwa urahisi. Kutokana na foleni na uduni wa huduma za usafiri wa umma watu wa kundi la kati, wamekuwa wakikimbilia kununua magari binafsi kwa ajili ya kwenda nayo kwenye shughuli zao kwa urahisi. Aidha, katika kuendeleza harakati za kupambana na tatizo la usafiri, Kampuni ya Transevents Marketing ya Tanzania kwa kushirikana na Kampuni ya Dutch Amphibious Transport Vehicles (DATV) ya Uholanzi inaendelea na mchakato wa kuleta usafiri wa mabasi ya abiria yenye uwezo wa kusafiri nchi kavu na majini. Mkurugenzi Mtendaji wa Transevents, Peter Nzunda anasema teknolojia hiyo ya mabasi ya nchi kavu na majini (amphibious) ina lengo la kupunguza tatizo la foleni kwenye barabara za Dar es Salaam hususan katikati ya jiji kwa kuwa mabasi hayo huweza kupita nchi kavu na majini. Hii ina maana kuwa hata katika maeneo yenye barabara zisizo nzuri au zenye tope, magari hayo huweza kupita hivyo kutosababisha foleni kama ambavyo hutokea sasa katika baadhi ya maeneo hasa mvua zinaponyesha na kuharibu barabara.