MCHAWI WA UNGO ADONDOKA, AGEUKA KUKU
Stori: Joseph Ngilisho, Arusha
HALI ya taharuki iliyoambatana na imani
za kishirikina iligubika Jiji la Arusha kufuatia mwanamke ambaye
hakufahamika jina kudondoka na ungo wa kishirikina asubuhi ya Ijumaa
iliyopita kisha ghafla kubadilika kuwa kuku mweupe mwenye mayai ndani
ya ungo, Uwazi limeona mengi.
Mamia ya wananchi katika eneo la
Kimandolu kando ya Barabara ya Arusha- Moshi walimiminika kushuhudia
tukio hilo lililojiri saa tatu asubuhi.
Akizungumza na Uwazi, shuhuda mmoja wa tukio hilo ambaye ni dereva wa bodaboda, Martin Mbise alisema:
“Nilikuwa kwenye shughuli zangu za kila
siku, ghafla niliona kitu kipana kikidondokea kwenye huu mtaro, ndani
yake nikamwona mtu amekaa akiwa uchi wa mnyama.
“Wengi tuliamua kusogelea eneo la tukio,
lakini kabla hatujakifika, mtu huyo alitoweka, badala yake mle mwenye
ungo mkawa na kuku mweupe na mayai zaidi ya kumi, tulishangaa sana:
Mbise alisema hali hiyo ilidumi kwa saa
mbili na nusu, ndipo wananchi hao wakaamua kumchoma moto kuku huyo baada
ya kumuua na kuyavunja mayai.
Hata hivyo, alisema haikuwa rahisi kuku
huyo kuungua licha ya kumwagiwa mafuta ya taa na petroli na wakachukua
uamuzi wa kumkatakata na kugawana nyama yake huku baadhi
yao wakikimbia hovyo na kulaani tukio hilo.
Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema
tukio hilo ni laana na anapaswa kuitwa mtumishi wa Mungu kwa ajili ya
kukemea pepo mchafu kwa maombi ya kiroho wakiamini mchawi huyo alikuwa
ana lengo la kuwadhuru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP
Lebaratus Sabas hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo, lakini
baadhi ya maafande waliofika katika eneo hilo walithibitisha.
No comments:
Post a Comment