KAULI KUMI(10) NA ZA KUSISIMUA ZILIZOVUTA HISIA ZA WENGI KWENYE BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA,ZISOME HAPA
Ni vigumu kueleza matukio yote yaliyotawala kauli na hisia za wengi kwa wiki nzima mjini Dodoma bila kuangalia michango ya baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.
Michango
hiyo ya mawazo katika mjadala kuhusu rasimu ya kanuni zinazopaswa
kuongoza kikao kwa siku 70 za kikao hicho, baadhi yake zilikuwa kali.
Mtikila,
ambaye ni mwenyekiti wa Democratic Party (DP), alitumia dakika tano
kutoa somo kwa wajumbe wa Bunge hilo kuhusu umuhimu wa kupiga kura ya
siri badala ya ile ya wazi.
Anasema
haki ya kupiga kura kwa siri haitofautiani na haki ya mtu kuwa na miguu
miwili na kwamba itashangaza akitokea mtawala akaamuru kila mtu awe na
mguu mmoja, halafu watu wakakaa kujadili.
“Wote tutaonekana tuna matatizo ya akili,” alisema Mch. Mtikila.
Alisema
Bunge Maalumu la Katiba litaingia katika hatia na aibu kwa kujadili
mambo ya msingi ya kidemokrasia ambayo pia yameainishwa katika katiba ya
sasa, likiwamo suala hilo la kura ya siri.
“Mwenyekiti
(akimlenga Pandu Ameir Kificho) tumekuchagua kwa kura ya siri siyo
kwamba tulikuwa wajinga kuliko wenzetu, hapana! Ni ‘democratic civility’
(ustaarabu wa kidemokrasia),” alisema.
“Ni
aibu waheshimiwa na hii nasema si jambo la mjadala kuna vitu vya
kujadili, lakini si haki ya kupiga kura kwa siri. Hii ni haki ya msingi
ya kidemokrasia,” alisema.
2. Profesa Ibrahim Lipumba (Mwenyekiti –CUF Taifa)
Mwenyekiti
huyo wa CUF alisema msingi wa kupiga kura ya siri ni kujaribu kuwalinda
wajumbe ambao wanaweza kupiga kura kinyume na misimamo ya vyama vyao au
makundi yao.
Akijenga
msingi wa hoja yake, Profesa Lipumba alisema hata Jaji Joseph Warioba
katika taarifa yake alisema moja ya taasisi zilizotoa maoni ni Baraza la
Wawakilishi lililopendekeza Serikali tatu.
“Tunadai
kura za siri kusudi kuwalinda hawa wenzetu ambao wametoa misimamo,
wakija kupiga kura hapa inaweza kuwapa matatizo huko walikotoka,”
alisema.
Aliongeza
: “Tunapolishabikia hili kuwa pasiwe na kura ya siri inaonekana wazi
pana ajenda ya kuwashughulikia watakaokwenda kinyume cha msimamo.”
3. Esther Bulaya (Viti Maalumu-CCM)
Bulaya,
tofuti na wajumbe wenzake wengi kutoka chama tawala (CCM), alionekana
kutoa mchango uliogusa hisia za wengi hasa pale alipoeleza bayana kuwa
hayuko tayari kuona ukandamizaji unafanyika kumlazimisha apige kura ya
wazi.
Akirejea
msimamo wa kura ya wazi unaoshabikiwa na wajumbe wengi wanaotokana na
chama chake, alisema hawezi kupiga kura ya aina hiyo wakati anajua
inamnyima uhuru wake.
“Nitasema
kweli daima, fitina kwangu mwiko. Ni lini na wapi katika uamuzi mgumu
kama huu kulifanyika kura za wazi kama wengi wanavyotaka,” alisema.
4. Pandu Ameir Kificho (Mwenyekiti wa Muda)
Naye
Kificho, ambaye pia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,
alionyesha kukerwa na baadhi ya vyombo vya habari hasa vilipolishikia
bango suala la posho.
“Kusema
kweli, jamii tunaichanganya mpaka jambo hili la kutupatia Katiba Mpya
lionekane ni la mchezo au tumekuja kudai posho. Nawataka wenzetu
(wanahabari) wawe makini sana juu ya jambo hili wasiupotoshe umma ili
kazi hii isiingie dosari,” alisema.
“Vyombo
vyote vya habari vizingatie kupata habari kwa uwazi na ukweli kutoka
kwa wanaohusika ili jamii yetu ya Watanzania ipate habari za kweli na
hilo la kupokea tu posho kwa kusoma magazeti tunalikanusha kwa nguvu
zote”.
Ndesamburo
aliwataka wajumbe wenzake kuacha ushabiki wa kisiasa na kutambua
wanatengeneza katiba itakayodumu miaka 50 ama miaka 10 ijayo.
“Tusilete
ushabiki. Nawaombeni sana tusilete ushabiki katika jambo hili. Hili ni
jambo zito. Hili ni jambo tunalolifanya kwa niaba ya Watanzania milioni
45 na sisi tumepata bahati tu; ni Mungu ametusaidia,” alisema.
6. Profesa Jumanne Maghembe (Waziri wa Maji)
Profesa
Maghembe alifananisha upigaji wa kura kwa siri kuwa sawa na ule
uliofanyika nchini Marekani wakati wa kashfa ya ufuska iliyokuwa
ikimkabili aliyekuwa rais wakati huo, Bill Clinton.
“Kule
Marekani walikuwa wakipiga kura ya kumwondoa madarakani Clinton kwa
madai ya kushikwa ugoni. Walipiga kura ya wazi kwa sababu lilikuwa jambo
kubwa la kumwondoa mtu madarakani,” alisema.
Profesa
Maghembe, ambaye pia ni Waziri wa Maji, aliwasihi wajumbe kutofautisha
upigaji kura wa mwenyekiti wa kijiji, diwani, mbunge na rais ambao
alisema wananchi hupiga kura za siri.
“Humu
ndani tunatafuta sheria mama ya nchi. Tumepewa jukumu hilo kwa niaba ya
Watanzania wote. Wao watapata nafasi ya kusema ndiyo au hapana. Sasa
tunajificha ili iweje, tunamficha nani?” alihoji.
7. Sheikh Hemed Jengo
Sheikh
Jongo alishauri Bunge Maalumu la Katiba kuwapa nafasi wajumbe wanawake
watakaokuwa katika hedhi, waruhusiwe kuapa bila kushika kitabu kitukufu,
Quran.
“Siku
nyingine kinamama wanakuwa katika siku maalumu (hedhi). Ni haramu kwa
mujibu wa dini kushika msahafu. Atakapojieleza kuwa hali yangu si nzuri,
basi aruhusiwe kuapa hivyo hivyo kwa heshima,” alisema na kuongeza:
“Hata
kwa wanaume wa Kiislaamu wakitaka kuapa wachukue udhu kwa sababu kitabu
chenyewe kinakataza kukishika bila ya udhu. Ndiyo yamini. Ndiyo maana
watu wengine hatuoni wanafanya vizuri kule nje kwa sababu wanajua
waliapa bila udhu na haikuwa yamini.”
8. Maria Sarungi Tshehai
Mwanaharakati
huyo alitumia fursa aliyopewa kuwaponda wajumbe wenzake waliokwenda
katika Bunge hilo kwa ajili ya kuwasilisha masilahi ya vyama.
“Hatuko hapa kwa ajili ya kuwasilisha vikundi mbalimbali. Tukianza hivyo itakuwa ni hatari sana katika Bunge hili,” alisema.
“Nianze
kwamba kitu kilichonifanya nitoke nje nilifutwa (na mtu ambaye
hakumtaja jina). Aliniambia wewe mbona unaonekana upo kwenye upande wa
chama fulani.”
9.Richard Ndassa (Mbunge wa Sumve)
Yeye
alionekana kukerwa na baadhi ya taarifa za vyombo vya habari kuhusu
suala la posho na kuvishtaki vyombo hivyo kwa mwenyekiti wa muda wa
Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho.
“Wabunge
wanachota milioni 129 kwa kikao cha dakika 30” na kingine kikisomeka,
“Wabunge walipwa milioni 130 kwa dakika 25; Bunge la Katiba vipande
vipande; wapewa posho kwa kusoma magazeti,” alisema akikariri vichwa vya
habari vya baadhi ya magazeti na kudai vinamkera.
10. Dk. Zainab Gama
Naye
mwanasiasa mkongwe, Dk. Zainabu Gama alikwenda mbali na kudai kuwa
baadhi ya wanaotaka kura ya siri wametumwa na watu ama wamekula rushwa
ndiyo maana hawataki kupiga kura ya wazi.
“Hatukuletwa hapa kimchezo mchezo. Simama, sema mimi uamuzi wangu huu kila mmoja akuone,” alisema.
MWANANCHI