Thursday 6 March 2014

Ngome ya al-Shabaab yadhibitiwa Somalia

 

Vikosi vya serikali ya Ethiopia na Somalia vimedhibiti mji ulio katikati ya Somalia uliokuwa mikononi mwa wanamgambo wa al-Shabaab, maafisa wameeleza.

Takriban watu 12 waliuawa katika mapigano makali katika mji wa Radboore lililokuwa likizozaniwa lililo mjini Bakol, wakazi wa eneo hilo wameshuhudia.
Vikosi vya Ethiopia ni sehemu ya Wanajeshi 22,000 wa Umoja wa Afrika (AU) wanaopambana na wanamgambo nchini Somalia.
Imeelezwa kuwa kudhibitiwa kwa mji wa Radhoore ni hatua muhimu kwa kuwa ilikua ngome kuu ya al-shabaab katika kutekeleza mashambulizi mjini humo.
Huu ni mji wa kwanza ambao al-Shabaab walipoteza tangu mwezi Septemba, mji wa Mahaday ulipodhibitiwa toka mikononi mwa al-shabaab.
Hivi sasa vikosi vinaelezwa kuwa vinaelekea mji wa Hudur ambao pia unadhibitiwa na al-Shabaab.
Wanamgambo hao wenye uhusiano na al-Qaeda, wanadhibiti eneo kubwa la katikati mwa Somalia.

No comments:

Post a Comment