Mapigano mapya mjini Juba
Wanajeshi wa waasi nchini Sudan Kusini
Wanajeshi watano wa serikali ya Sudan Kusini wameuawa kufuatia mapigano makali ndani ya kambi moja ya kijeshi mjini Juba.
msemaji
wa jeshi la nchi hiyo amesema kuwa wanajeshi wengine watatu
walijeruhiwa kwenye mapigano hayo iliyotokea katika kambi ya jeshi ya
Jebel.
Mapigano kama hayo ndani ya kambi hiyo kati ya makundi hasimu yalisababisha mgogoro mkubwa wa kisiasa nchini humo.
Mkaazi
mmoja wa Juba ameiambia BBC, kwamba moshi mweusi ulionekana ukitapakaa
angani juu ya kambi hiyo karibu na chuo kikuu cha Juba na kwamba watu
wameonekana wakilitoroka eneo hilo.
Akiongea
muda mfupi kwenye runinga ya taifa muda mfupi baada ya mapigano hayo
kuanza, Brigadier General Malak Ayuen Ajok amesema kuwa waliouwa ni
wanajeshi waatiifu kwa serikali.
Amesema
mapigano hayo yalisababisha na mvutano kati ya wanajeshi ambao walikuwa
wakizozana kuhusu kucheleweshwa kwa mishahara yao.
Ajok, ameongeza kuwa hakuna dalili yoyote ya mapigano hayo kusambaa katika maeneo mengine ya mji huo.
Lakini watu wengi wanaoishi karibu na kambi hiyo ya wamekimbia makwao na kutafuta hifadhi katika piga makanisa na shule.
Mzozo
wa Sudan kusini ulianza mjini Juba, mnamo mwezi Disemba mwaka uliopita
kufuatia hali ya wasiwasi kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu
wake wa rais Riek Machar lakini ukaenea kote nchini humo.Chanzo BBC
Swahili
No comments:
Post a Comment