Juhudi za Kerry zagonga mwamba Paris
Katika njia Panda: Sergei Lavrov na John Kerry.
Juhudi za marekani kuwakutanisha
kwa mara ya kwanza ana kwa na mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa
Urusi na Ukraine kuhusu mzozo unaoendelea katika jimbo la Crimea
zimegonga mwamba.
Ingawa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni
Marekani John Kerry amekanusha kwamba palikuwa na nia ya kumkutanisha
mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov na waziri mpya wa mashauri ya nchi za wa
Ukraine Andrii Deschchytsia iwapo wawili hao wangekutana mjini Paris
ingekuwa ni mafanikio makubwa ya kidiplomasia.Sergei Lavrov alikataa kukutana na waziri huyo mpya wa Ukraine kwa sababu Urusi haitambui utawala mpya wa mjini Kiev. Akizungumza mjini Paris Bwana Deschchytsia amesema licha ya vuta nikuvute hiyo anaamini kwamba kuna dalili ya mafanikio katika mashauri.
" Kwa hiyo baada ya kuwa hapa siku nzima mjini Paris, inaonekana kwamba tunaendelea na mashauri yetu na tunaamini kwamba tutapata mwafaka. Ninaelekea mjini Brussels kukutana na waziri mkuu kujadili hatua zaidi za kuchukua. Shukran."
Na alipoulizwa na mmoja waandishi wa habari ni kwa nini hakuweza kukutana na waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi Sergey Lavrov hivi leo, bwana Deschchytsia alijibu- ''kamuulize Lavrov mwenyewe.''
Mwanajeshi wa Ukraine akilinda meli ya kivita iliyozuiliwa na Urusi katika bandari ya Sevastopol.
Waziri wa mashauri ya nchini za kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius kadhalika alielezea matumaini ya mazungumzo hayo kufanikiwa.
" Tumekubaliana kuendelea na mashauri kwa sababu mambo bado na hali sio rahisi anasema bwana Fabius. Lakini tunayo furaha kwamba siku ya leo mjini Paris imeturuhusu kuanzisha mikakati.''
Kwa upande mwingine rais wa Urusi Vladmir Putin alifanya mazungumzo kuhusu mzozo huo na chanzela wa Ujerumani Angela Merkel kwa njia ya simu.
Wakati huo huo Mwakilishi mkuu wa Umoja wa mataifa huko Crimea, Robert Serry, amelazimika kukatiza ujumbe wake baada ya kutishiwa na watu waliojihami alipokuwa akitoka katika makao makuu ya jeshi la wanamaji la Ukraine katika bandari ya Simferopol.
No comments:
Post a Comment