Pinda, Werema wabishana utaratibu wa hotuba
Dodoma. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Jaji Frederick Werema wamepingana hadharani kuhusu anayepaswa
kuwa wa kwanza kuhutubia Bunge kati ya Rais Jakaya Kikwete au
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Mabishano hayo yalitokea juzi wakati wajumbe wakichangia Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, mjini Dodoma.
Ubishi baina ya vigogo hao wa serikali ulizuka
baada ya Jaji Werema kusema kuwa kanuni ya saba inaelekeza Jaji Warioba
ndiye anayepaswa kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba, lakini Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba haijasema kama Rais anapaswa kuhutubia kwenye
ufunguzi wa Bunge la Katiba.
Pinda aliingilia mabishano hayo kwa kuelekeza kuwa
Jaji Warioba atawasilisha rasimu hiyo na kufuatiwa na hotuba ya
ufunguzi itakayotolewa na Rais Kikwete.
Hoja hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka.
Hata hivyo, Mjumbe wa Kamati ya Kanuni, Ismail
Jussa alisema hakuna kipengele cha sheria kinachozungumzia hotuba ya
Rais ambacho katika utungaji wa kanuni kingefanywa kuwa na kifungu cha
peke yake.
No comments:
Post a Comment