Makahaba watumia Vibaya Hijab Kenya
Makahaba katika baadhi ya sehemu za mji mkuu wa Kenya
, Nairobi, wametupilia Mbali vazi la 'Mini skirt na kuanza kutumia
Hijab kama njia ya kuwavutia wateja wao, jambo ambalo limekashifiwa
vikali na wakuu wa dini ya Kiislamu.
Hijab huvaliwa na wanawake wa Kiislamu kama
ishara ya kumcha Mungu, lakini makahaba katika mtaa wa Eastleigh,
viungani mwa Nairobi wanatumia Hijab ili kuwafanya wateja wao kudhania
kua wanatoka sehemu za Pwani.Taarifa hii ni kwa mujibu wa mtandao wa shirika la habari la Nation mjini Nairobi.
Mwanamke mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa yeye hupata wateja maradufu kwani huvalia vazi hilo la Hijab, wengi wa wateja wake wakimuona kama mwenye nidhamu.
Uchunguzi ulibaini kuwa wanawake wasio wa kiislamu wanavalia vazi hilo ili kuwavutia wanaume ambao wanaamini kuwa wao wana maadili zaidi ya wale wanaovalia nguo fupi au 'Mini Skirt'.
Nguo fupi ni mavazi yaliyozoeleka kwa makahaba sehemu nyingi duniani
Hata hivyo chama cha makahaba nchini Kenya kimewatetea makahaba hao wanaotumia hijab huku likidai kwamba wanafanya hivyo ili kukidhi mahitaji ya wateja wao.
Mratibu wa muungano huo, Bi Phelister Abdalla, aliiomba serikali kuhalalisha ukahaba kwa madai ya viwango vya juu vya ukosefu wa ajira.
Mahojiano na makahaba katika mtaa wa Eastleigh yalibaini kwamba wanaume hawakuwa na haja ya wanawake wenye kuvalia nguo fupi badala yake wakipendelea wanawake wa kiislamu na wale wa kutoka Ethiopia.
No comments:
Post a Comment