Zanzibar yashauriwa kurekebisha Katiba
Alisema wakati Katiba ya Zanzibar ikieleza hivyo, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya 1 inaelezaa kuwa Tanzania ni nchi moja na eneo lake la mipaka ni kuanzia Tanzania Bara hadi Visiwani
Zanzibar. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
(SMZ) imeshauriwa kufanya marekebisho ya Katiba kabla ya Uchaguzi Mkuu
Mwaka 2015 ili kuondoa vifungu vinavyogongana na Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Ushauri huo umetolewa na mwanasiasa mkongwe wa
Zanzibar, Ali Hassan Khamis wakati akiwasilisha mada juu ya hali ya
kisiasa na mchakato wa Katiba ya Muungano katika kongamano
lililoandaliwa na Jumuiya za CCM, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Tawi la
Kiembesamaki Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
Alisema migongano inayojitokeza katika Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar imetokana na marekebisho ya 10 ya Katiba ya
Zanzibar ya mwaka 1984 iliyogongana na Katiba ya Muungano na kusababisha
mjadala mkubwa katika mchakato wa mabadiliko ya katiba unaoendelea.
Alisema marekebisho hayo ya Katiba ya Zanzibar
yameongeza migongano hasa sura ya 1(1) inayoeleza kuwa Zanzibar ni nchi
ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba
pamoja na visiwa vidogo vilivyozungukwa na bahari yake, ambayo kabla ya
Muungano wa Tangayika na Zanzibar ilikuwa ikiitwa Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar.
Alisema wakati Katiba ya Zanzibar ikieleza hivyo,
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya 1 inaelezaa kuwa
Tanzania ni nchi moja na eneo lake la mipaka ni kuanzia Tanzania Bara
hadi Visiwani.
Aliwaeleza washiriki hao kuwa kifungu cha 2(a) cha
Katiba ya Zanzibar kimempa uwezo Rais wa Zanzibar kuigawa Zanzibar
katika mikoa na wilaya kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977.
Alisema marekebisho hayo ya 10 yamechangia kwa
kiwango kikubwa kuibua migogoro ndani ya Muungano na kutaka Katiba ya
Zanzibar iandikwe upya na wananchi wapewe nafasi ya kuijadili na kuamua.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Vilevile alieleza katika marekebisho hayo ya 10
kuna vitu viliondolewa lakini havikuwa na ulazima kama wakuu wa mikoa
kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (BLW), wakati ni watendaji wakuu
wa shughuli za Serikali katika kuwahudumia wananchi kwenye maeneo yao.
“Wakati umefika katiba yetu ya Zanzibar iangaliwe
upya iendane na Katiba ya Jamhuri ya Muungano vinginevyo tutaendelea
kuendeleza migogoro na kuathiri msingi mzima wa Muungano na Mapinduzi ya
Zanzibar,” alisema Ali Hassan Mkuu wa Wilaya ya Kati wa zamani visiwani
humo.
Akifafanua zaidi alisema hata muundo wa Serikali
ya Umoja wa Kitaifa (SUK), una kasoro Zanzibar kutokana na sera ya CCM
kuwa ni moja kati ya Zanzibar na Tanzania Bara lakini mfumo huo wa
Serikali umezingatiwa upande marekebisho hayo ya kati mmoja wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
“Chama chetu ni kimoja, ni sehemu gani sera yetu
imesema CCM ikishinda itaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa wakati hilo
Tanzania Bara halipo,” alisema.
No comments:
Post a Comment