Thursday 27 March 2014

Bei ya gesi kupanda maradufu Ukraine

Serikali ya mpito ya Ukraine imesema itaongeza bei ya gesi kwa watumiaji wa ndani kwa asilimia 50 zikiwa jitihada za kuhakikisha kuwa wanafanikiwa kupata mkopo kutoka Shirika la fedha duniani, IMF

 

Shirika la taifa la nishati ya gesi, Naftogas limetangaza nyongeza ya gharama hizo kuanza kutekelezwa tarehe mosi mwezi Mei.
Ukraine hununua gesi nusu ya gesi yake ya asili kutoka kampuni ya Gazprom ya Urusi, kisha huiuza kwa watumiaji wake kwa gharama nafuu.
IMF halikadhalika inaitaka Ukraine kupambana na vitendo vya rushwa na kusitisha mchakato wa Benki kuu ya Ukraine kusaidia fedha ya nchi hiyo.
Siku ya jumanne, waziri wa fedha wa nchi hiyo Olexander Shlapak alisema Ukraine inahitaji kiasi cha Pauni bilioni 9-12 kutoka kwa IMF.
Jarida la Financial Times limeripoti kuwa uamuzi uko mbioni kufikiwa kuhusu kiasi cha fedha cha takriban dola za kimarekani bilioni 15
ambacho Ukraine inatakiwa kujiokoa na kwamba maamuzi hayo yatatangazwa rasmi Alhamisi.
Makubaliano kati ya Ukraine na IMF ni muhimu wakati huu ili kuweza kupata misaada zaidi kutoka kwa Jumuia ya Ulaya na Marekani.
Msaada wa kifedha unahitajika haraka wakati nchi hiyo ikiwa imelazimika kutumia hifadhi ya fedha za kigeni,huku uchumi nao ukitarajiwa kuanguka kwa 3% mwaka huu.
Wizara ya fedha nchini humo pia inatarajia msaada kutoka kwa Marekani japo kiasi kamili kinasubiri mjadala na bunge la Congress.

 

No comments:

Post a Comment