Rwanda na A.Kusini kusuluhisha mgogoro
Rais Jacob Zuma wa Afrika-Kusini na Paul Kagame wa Rwanda wamekubaliana mjini Luanda Angola, kuanzisha mazungumzo ya pamoja ya kumaliza mzozo wao wa kidiplomasia
Jaribio la kumuua Kayumba Nyamwasa lilitibuka Afrika Kusini
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulianza kuzorota pale Rwanda
ilipowafukuza maafisa sita wa ubalozi wa Afrika Kusini, saa chache baada
ya Afrika Kusini kuwatimua wanadiplomasia watatu wa Rwanda kuondoka
nchini humo karibu wiki tatu zilizopita.Lakini Serikali ya Rwanda ilisema hatua ya kuwatimua maafisa sita wa ubalozi wa Afrika Kusini mjini Kigali ni ya haki na ilizingatia uchokozi ambao ulianzishwa na serikali ya Afrika Kusini yenyewe kwa kufukuza maafisa watatu wa ubalozi wa Rwanda.
Rwanda ilisema kuwa Afrika Kusini ndio ilianza uchokozi kwa kuwatimua mabalozi wake watatu
Nyumba yake iliharibiwa huku komputa na baadhi ya nyaraka zilichukuliwa.
Mkutano wa usalama uliofanyika mjini Luanda ulijadili hali kati ya nchi hizo mbili huku viongozi hao wawili wakikikutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu mzozo huo kutokea.
Rais Zuma alisema kuwa wamekubaliana kusuluhisha mgogoro huo na pia kupata taarifa ya pamoja ili kuweza kusuluhisha tofauti kati yao.
Kadhalika Rais Zuma aliongeza kwamba serikali yake inatekeleza wajibu wake wa kimataifa kwa kuwapa hifadhi watu wanaoomba. Viongozi hao wawili wamekubaliana kukutana kwa ajili ya kuzungumzia swala hilo baadaye.
No comments:
Post a Comment