Tuesday 25 February 2014

Watoto milioni moja wauawa katika Vita

 
Watoto wateseka kutoka na vita  
Watoto Milioni moja hufa siku yao ya Kuzaliwa
Shirika la Misaada kwa watoto, Save the Children, linasema kuwa watoto milioni moja hufariki dunia kila mwaka katika siku yao ya kwanza ya maisha.
Katika ripoti mpya ya shirika hilo la misaada kwa watoto linasema vifo vya watoto wachanga vimesalia kuwa moja ya aibu za dunia ya sasa.
Hali ya watoto ni mbaya zaidi hasa katika mataifa yanayokabiliwa na mizozo.
Mwandishi wa BBC aliye Sudan Kusini, Anne Soy, amesema kuwa katika mazingira ya sasa ya Sudan Kusini, watoto na wanawake, hasa wale waja
wazito wanaokabiliwa na athari nyingi za vita vinavyoendelea nchini humo.
Amesema kuwa kutokana na vita watoto, walioandamana na wazazi wengine wakiwa pekee, wanaungana na akina mama kutembelea mwendo
mrefu ili kujiepusha na vita vya kikabila vinavyoendelea nchini.
Miundo msingi katika Sudan Kusini, kama vile hospitali ni chache sana jambo ambalo linatatiza maisha ya wanawake na watoto.
Katika hospitali ya mji wa Nimule kwenye mpaka wa Sudan Kusini na Uganda Kuna vitanda 174 pekee hospitalini idadi ambayo haiafikiana kamwe
na maelfu ya wagonjwa na wahasiriwa wa vita .
Save the children inasema kuwa vita vinawaathiri zaidi watoto huko Syria, Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Shirika la Save the Children linasema kuwa vifo hivi vingi vinaweza kuzuiliwa.


No comments:

Post a Comment