Wednesday, 6 August 2014

Hii ndio siri ya Diamond kutomuacha mamaa yake kila aendapo.
10584511_1649508395274921_1890441585_n

Kwa jinsi Diamond anavyoonekana akiwa na ukaribu sana na mama yake mzazi toka day one, wengi wamejaribu kuhoji sana ni nini hasa siri iliyo nyuma ya ukaribu uliopitiliza wa Diamond kwa mama yake, ila siri iliyopo inarudisha nyuma sana kipindi ambacho Diamond akiwa ndio ana-hustle kutafuta njia ya kutokea katika fani hii ya muziki wa Bongo fleva, kipindi hiko ambacho Tanzania haitambui kabisa kama kuna mwanamuziki anayejiita Diamond Platnumz.
p

Kuna mambo mengi sana ambayo bila msaada wa mama yake mzazi, hivi leo kusingekuwa kuna jina linalowakilisha Bongo huko ugaibuni kama Diamond platnumz, tukio moja ambalo hata Diamond mwenyewe hawezi kusahau katika historia ya muziki wake, ni pale mama yake mzazi alipojitolea pete yake ya dhahabu na kuiuza ili mwanaye ambaye ni Diamond apate hela ya kuingia studio na kurekodi track yake ya kwanza.
10576138_770511582969037_1834689818_n

Naamini ni wazazi wachache sana wanaweza kufanya jambo kama hili, mbali na kupitia vizuizi vingi katika safari yake ya muziki, mama yake mzazi ndio aliyekuwa rafiki wake wa karibu aliyefanikiwa kumuongoza Diamond tena bila kukata tamaa, hadi hii leo kufikia mafanikio aliyonayo ambayo hata Raisi wa nchi yake(mH.Jakaya) hawezi kusahau jina la Diamond pale anapojarbu kuongelea sanaa ya muziki huu wa Tanzania. Ukaribu huo unaweza kuonekana ni umetoka mbali, ni zaidi ya mama, ni mtu ambaye amechangia mafanikio makubwa katika muziki wake.
1524981_665641786790972_1806280682_n

Hii ni nyingine tena kutoka Nuh na Shilole?taarifa ikufikie kumbe wameachana.

 Embedded image permalink



Stori ya Nuh Mziwanda kujichora tatoo yenye jina la Shilole ilisambaa sana na wengi walikua wakijiuliza siku ikitokea wameachana itakuaje hasa upande wa Nuh ambaye ndiye aliyejichora tatoo hiyo.
nuh
Maelezo ya Nuh Mziwanda yamedai kuwa sababu zilizosababisha waachane ni msg ambayo aliikuta kwenye simu ya Shilole ambayo inasemekana ilitumwa na mwanaume,Nuh alipomwambia Shilole apige alionekana kunikanyanga.
Nuh Mziwanda kaongea na Soudy Brown kwenye You heard na kazungumza mambo mengi ambayo yametokea kwenye uhusiano wao.

Tuesday, 5 August 2014



ALIKIB AFUNGUKA KUHUSU LULU. AONGELEA PIA TUHUMA ZA KUMTOA BIKRA JACKLINE WOLPER

HII ni exclusive! Kwa mara ya kwanza, staa anayeitikisa nchi kwa sasa na wimbo wake wa Mwana, Ali Kiba amefunguka kuwa mwigizaji kiwango Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ anafaa kuwa mke (wife material) huku akiweka wazi sifa kibao alizonazo, Wikienda liko bize kukujuza.
Staa anayeitikisa nchi kwa sasa na wimbo wake wa Mwana, Ali Kiba ndani ya ofisi za global.
Kiba ambaye hivi karibuni ameibua mijadala mingi katika mitandao ya kijamii, usafiri wa umma na kwenye baa juu ya ujio wake mpya akisemekana kurudia kiti chake ambacho alikikalia Mbongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’ kwa muda, mwaka 2010 aliwahi kuripotiwa katika magazeti pendwa kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na Lulu ambaye wakati huo alikuwa na umri chini ya miaka 18!
LULU ANAFAA KUWA MKE
Akizungumza mbele ya kinasa sauti cha Globa TV Online, Bamaga-Mwenge jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Kiba ambaye anatarajia kuangusha shoo ya kihistoria Agosti 8, mwaka huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, alisema Lulu anafaa kuwa mke kwa vile ni mchapakazi sifa ambayo mke mwema anapaswa kuwa nayo.
AMMWAGIA SIFA
Kiba alisema Lulu anajua kuhangaika, anajua kupambana kusaka pato lake kihalali kupitia mauzo ya sinema zake anazozizalisha kitu ambacho kinawashinda mabinti wengi na kuangukia katika biashara ya kuuza miili (ukahaba).
Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ akiwa na Ali Kiba.
Licha ya kummwagia sifa hizo, kipindi hicho alichokuwa akitajwa kuwa naye, Lulu alikuwa na matukio ambayo hayakuwa na maadili lakini Kiba hayo hakuyatilia maanani.
Mwandishi: Unafikiri Lulu ni ‘wife material’ (mke mwema) ambaye unaweza kumweka ndani akalea watoto na kuijenga familia bora?
Kiba: Yeah! Anafaa kuwa mke, ni binti anayejituma, mchapakazi, mtafutaji. Kwangu mimi mtu wa namna hiyo ndiyo anafaa kuwa mke.
Mwandishi: So, unataka kutuambia kwamba unaweza kumuoa?
Kiba: Sijasema hivyo mimi, nimesema anafaa kuwa mke.
ACHOMOA KUBANWA KISHERIA
Licha ya kuchomoa ishu hiyo ya uhusiano, mapaparazi wetu walimbana zaidi staa huyo afafanue kwa nini alitajwa yeye na si msanii mwingine huku ikidaiwa kuwa, Lulu hakuwa ametimiza miaka 18 hivyo kubanwa kisheria (ya watoto na kujamiiana).
“Sijatembea naye ndiyo maana unaona hata sheria haijanihukumu, endapo ningekuwa nimetembea naye, basi sheria ingeweza kunitia hatiani na ningefungwa jela,” alifafanua Kiba.
  'Kanumba The Great' enzi za uhaim wake.
AWASHANGAA WANAOMSHANGAA
Kiba aliongeza kuwa, anashangaa sana kuona watu wanamsema vibaya yeye kupendwa na Lulu.
“Lulu ni msanii mwenzangu, anapenda kazi zangu na mimi napenda za kwake. Ni rafiki wa kawaida, hakuna kitu kingine cha ziada. Nawashangaa wanaozusha ya kuzusha, hivi kwani kuna tatizo Lulu akinipenda? Sidhani kama ni kosa, ana haki ya kunipenda kutokana na muziki wangu.
“Unajua muziki mzuri huwa unapenya automatically, huwezi kuzuia hisia za muziki, mtu unaweza ukawa humpendi msanii f’lani lakini ukapenda muziki wake, unajikuta tu unampenda, unaanza kuimba nyimbo zake,” alisema Kiba.
KUMBUKUMBU MBICHI
Juzikati wakati Kiba anatambulisha nyimbo zake mbili kwa mpigo (Mwana na Kimasomaso), Lulu, kupitia mtandao wa Instagram alitupia maneno ya kummwagia sifa staa huyo, liliibuka kundi ambalo linatajwa kuwa ni wafuasi wa mwigizaji Wema Sepetu ‘Team Wema’ na kuanza kumshambulia kwa maneno machafu.
KIBA AFUNGUKA
Akizungumzia ishu hiyo, Kiba alisema waliofanya hivyo hawakumtendea haki Lulu kwani ana haki ya kueleza hisia zake pale anapoguswa na muziki mzuri.
“Hawajatenda haki kwa sababu Lulu ni binadamu kama walivyo wengine, ana haki ya kupenda kitu kizuri,” alisema Kiba.
KUHUSU KIFO CHA KANUMBA
Kiba akizungumzia juu ya kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa nyota wa sinema Bongo, marehemu Steven Kanumba ambapo alidaiwa kunaswa kwa meseji za mapenzi alizozituma kwa Lulu ndiyo zilizosababisha mtifuano ambao ulisababisha kifo cha Kanumba, alikana madai hayo.
“Si kweli, sikuwa nimewasiliana na Lulu siku hiyo kabla ya tukio. Nakumbuka nilikuwa safarini, baada ya tukio nilimpigia Lulu kutaka kujua ukweli wa taarifa za kifo kwa sababu marehemu alikuwa mtu wangu  wa karibu kama alivyo Lulu,” alisema Kiba.
AMGUSIA WOLPER
Kwenye mahojiano hayo, mkali huyo alizungumzia ishu ya mwigizaji, Jacqueline Wolper kukiri kwamba Kiba ndiye mwanaume aliyemtoa usichana wake kwenye simulizi iliyochapishwa katika Gazeti la Championi hivi karibuni.
“Mh! Aliwahi kukiri? Daah! Sijui bwana… Wolper ni mtu wangu wa karibu kama alivyo Lulu,” alisema kwa mkato Kiba.Juzi, Lulu alitafutwa na mapaparazi wetu ili  azungumzie ukaribu wake na Kiba, lakini simu yake muda mwingi iliita bila kupokelewa (tunaamini atasoma hapa, tunaendelea kumtafuta ili afunguke).
Ili kupata mahojiano hayo kwa kirefu zaidi, fuatilia tovuti ya

Friday, 1 August 2014

Picha hizi za Wema Sepetu na Martin Kadinda zina make headline kutizamwa kwenye mitandao 

Wema Sepetu na Martin Kadinda wamekuwa karibu sana hasa ukizingatia kuwa Kadinda amekuwa manager wa Wema kwa muda mrefu.Hizi ni picha alizo share Wema siku za nyuma ila hadi leo zimekuwa zina make headline kwenye mtandao wa Instagram.

  

Baada ya Wema kueleza alivyo m-miss, Hizi ndizo picha alizo share Ommy Dimpoz akiwa na Wema 

Siku tano zilizo pita kupitia mtandao wa Instagram, Mwigizaji wa filamu hapa Tanzania, Wema Sepetu aliandika kuwa ame mmiss msanii wa nyimbo za bongo fleava Ommy Dimpoz.
Huyu binadamu jamani tokea nimuone kwenye Mtv Awards sijamuona mpaka leo... Kiukweli nimemmiss saaaaana.... Mpuuzi wangu mwenyewe... Miss u shem lake... @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz

Haya ndiyo majibu ya Ommy Dimpoz ambapo ame share picha wakiwa pamoja na Wema Sepetu.


 

Monday, 19 May 2014

5 wauawa katika mlipuko Nigeria

Bomu lililolipuka katika mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria limewaua watu 5 na kuwajeruhi wengine wengi.
Shambulio hilo limefanywa katika eneo linaloaminiwa kuwa na waumini wengi zaidi wa dini ya kikristu, ambao wamekuwa wakilengwa mara nyingi na wapiganaji wa Boko Haram.
Mwandishi wa BBC mjini Abuja Will Ross anasema kuwa eneo hilo lililolengwa linajulikana kama Sabon Gari. Watu wengi walikuwa kwenye migahawa ya vileo na kwenye barabara. Amesema kuwa kilichosalia kwenye gari lililokuwa na bomu hiyo ni injini pekee.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja mji wa Kano umepumzika kutokana na mashambulio, hasa kwasababu ya oparesheni kali iliyofanywa na maafisa wa usalama kuwasaka wanamgambo hao wa Boko Haram.


Mlipuko wa bomu Nigeria 

Mashambulio ya awali

Mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kituo cha basi kilishambuliwa kwa bomu na awali mwaka wa 2012, Boko Haram walifanya shambulio baya zaidi lililowaua zaidi ya watu 150 katika msururu wa milipuko.
Kundi hilo bado linawazuilia wasichana zaidi ya 200 wa shule, lililowateka kutoka kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa Nigeria mwezi mmoja uliopita.
Nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Ufaransa na Marekani wameahidi kutuma wanajeshi kusaidia kuwakomboa wasichana hao.
Nao viongozi wa Afrika wanaokutana mjini Paris wametangaza 'vita' dhidi ya Boko Haram na kuahidi kushirikiana ki-intelijensia na kijeshi, kupambana na Boko Haram.


 

Wednesday, 7 May 2014

Rais Kikwete afungua mkutano wa Majaji Wanawake Arusha

      
mpya 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Asha Rose Migiro,Jaji Mkuu Mohamed Othman Chande,pamoja na Rais wa Chama Cha Kimataifa cha Majaji Wanawake wakiimba wimbo wa taifa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 12 wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha AICC.Mkutano huo ulifunguliwa na Rais Kikwete.22bh nhnmhjm
Baadhi ya majaji wanawake wanaoshiriki Mkutano wa 12 wa Chama Cha Kimataifa cha Majaji  wanawake unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano mjini Arusha