Mbunge wa Arumeru Mshariki , Joshua Nassari aumbuka bungeni
Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Joshua Nassari, juzi alijikuta akiumbuka bungeni baada ya kushindwa kutaja kanuni aliyoitumia, kuomba mwongozo.
Hali hiyo ilitokea muda mfupi kabla ya wajumbe kupiga kura za kumchagua Mwenyekiti wa Bunge hilo.
Kuumbuka kwa
mjumbe huyo ambaye pia ni Mbunge wa Arumeru Mshariki, kulitokana na
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho, kumtaka kutaja
kanuni aliyoitumia.
Hata hivyo, baada
ya kusita kwa muda Nassari bila kutaja kanuni aliyoitumia, alisema
wajumbe wengi hawajasikia utaratibu unaotumika katika upigaji kura kwa
sababu walichelewa kwenye msongamano wa watu getini.
“Wengi wetu
tumeingia tukiwa tumechelewa kwa sababu wengi tunapita katika geti
moja. Ningependa ufafanuzi wako kuhusu aina ya kura tunayokwenda kupiga
ni ya wazi au ya siri,”alisema.
Hata hivyo, kificho alimjibu kuwa kura zitakazopigwa kumchagua mwenyekiti zitakuwa ni za siri.
Hatua hiyo
imekuja muda mfupi baada ya Bunge hilo kupitisha kanuni za uendeshaji
wake ambapo hata hivyo nyingine bado zimekuwa na mgongano wa maridhiano
kwa baadhi ya wajumbe kutaka ufafanuzi zaidi.
No comments:
Post a Comment