Monday, 3 March 2014

SHY-ROSE AIOMBA SERIKALI YA TANZANIA KUWEZESHA WATANZANIA WAIFAHAMU EAC NA FAIDA ZAKE

1069410_488216681262565_60269170_n
Katibu wa Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Shy-Rose Bhanji (pichani) amerejea nchini baada ya ziara ya siku 10 ya Wabunge wa EALA nchini Kenya na hicho ndicho alichokisema kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nimerejea nchini baada ya ziara ya siku 10 nchini Kenya. Ziara hii ya wabunge wa EALA ilikuwa kwa mwaliko wa Serikali ya Kenya lengo likiwa kuhamasisha wananchi wa Kenya kupata ufahamu mkubwa juu ya Mtangamano wa Jumuiya na faida zake. Tulipata nafasi ya kuonana na wananchi, wafanyabiashara, wabunge, maseneta, magavana, asasi za kiraia na makundi mengine.

Ziara hii imenifungua macho zaidi kwamba bado tuna kazi kubwa mbele yetu kuhakikisha kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inakuwa ni ya Wananchi (people Centred Integration).

Kama nilivojionea mwenyewe kwa upande wa maeneo mbalimbali tuliyoyafikia bado mwamko wa ufahamu wa masuala ya EAC mdogo sana na kiu wa kuifahamu ni kubwa.

Hata hivyo Serikali ya Kenya kwa kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanashiriki kikamilifu juu ya masuala ya Jumuiya imefufua mpango huu wa wabunge wa EALA kufika Kenya kuendelea na zoezi la uhamasishaji.
Ni imani yangu kwamba na Serikali ya Tanzania itaiga mfano huu mzuri wa kuwaalika wabunge wa EALA kufika nchini ili kuwafikia makundi mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuhamasisha. Hata kwa upande wa Tz bado ufahamu wa wananchi wengi zaidi juu ya masuala ya Integration ni changamoto kubwa.

Lengo kuu la uanzishwaji wa EAC ni kuinua hali ya kiuchumi kwa wananchi wa EA ambao sasa ni takriban millioni 140. Na iwapo mwamko wa wananchi ni mdogo basi lengo hili litachukua muda mrefu sana kufikiwa au kutokufikiwa kabisa.

 

MADEREVA WA MALORI ZAIDI YA 300 WAGOMA KUENDELEA NA SAFARI KATIKA BARABARA KUU ITOKAYO DODOMA HADI MWANZA BAADA YA MWENZAO KUVAMIWA

 

Madereva wa malori zaidi ya mia tatu wamegoma kuendelea na safari katika barabara kuu itokayo Dodoma hadi Mwanza baada ya dereva mwezao aliyekuwa akiendesha lori kuvamiwa na majambazi katika eneo la kisaki manispaa ya Singida.


Wakiongea na ITV /Radio one madereva ambao wamekutwa katika eneo hilo wameomba jeshi la polisi kufanya doria mara kwa mara eneo hilo kwani kumekuwa na matuki yanayo jirudia ya utekeji wa magari kwa kuweka mawe makubwa barabarani na kuwajeruhi madereva jambo ambalo lina tishia amani kwa watumiaji wa barabara.

Madereva wa malori baada ya kufunga barabara naibu waziri wa Afrika mashariki Dr. Abdulla Abdulla alikumbwa na adha hiyo na kusema ni haki ya kikatiba kwa madereva kugoma kwa kudai haki zao, kutokana na hali hiyo amewahaidi madereva kupeleka kilio chao katika mamlaka husika ili kuweza kutatua tatizo lao na kukomesha vitendo vya uvamizi wa magari katika eneo hilo .

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida SACP Geofrey Kamwela amesema madereva waliamua kusimama barabarani bila sababu yeyote kwa muda wa zaidi ya masaa matatu na kusababisha foleni kubwa ambapo kwamujibu wa sheria za usalama barabarani walikuwa wamefanya kosa ,lakini baada ya viongozi kufika na kuwasikiliza waliamua kuendelea na safari.

Naye dereva wa lori bwana Agustino Mbawala aliye tekwa, akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida akiongea kwa shida huku akiwa na maumivu makali amesema aliona mawe makubwa barabarani na kuamua kusimama na kukimbia lakini wali mvamia na kumpiga hatimaye kumpora fedha na simu 

Friday, 28 February 2014

Viwanja vya ndege vyadhibitiwa Crimea

Waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine amesema majeshi ya Urusi yamekuwa yakiweka vizuizi katika uwanja wa ndege wa Sevastopol uliopo katika jimbo la Crimea.

 

Watu wenye silaha wakilinda doria uwanja wa ndege Simferopol, Crimea, Ukraine

Waziri huyo wa Ukraine, Arsen Avakov ameita uwepo wa majeshi ya Urusi katika jimbo hilo kuwa "uvamizi wa kijeshi".
Watu hao wenye silaha pia wameutwaa uwanja mwingine mkubwa wa ndege wa Simferopol, uliopo pia Crimea Ijumaa asubuhi.
Uhusiano kati ya Urusi na Ukraine umeyumba tangu kuondolewa madarakani kwa Rais wa Ukraine, Viktor Yanokovych, ambaye kwa sasa yuko nchini Urusi.
Uhasama huu umedhihirika zaidi katika jimbo la Crimea, nchini Ukraine, ambalo wakaazi wake wengi ni Warusi.
Siku ya Alhamisi, watu wenye silaha wenye mwelekeo wa Urusi, walivamia ofisi za bunge la Simferopol, na kuliondoa baraza la sasa la mawaziri na kumchagua waziri mkuu mpya.
Bado haijafahamika watu hawa wenye silaha katika mji wa Simferopol waliowasili katika uwanja wa ndege mapema ni kina nani.
Licha ya kuwepo kwao, inasemekana shughuli zinaendelea kama kawaida katika uwanja wa ndege wa Simferopol.
Watu walioshuhudia tukio hilo wameliambia shirika la habari la Ukraine, Interfax, kuwa watu wapatao 50 waliwasili katika uwanja wa ndege wa Simferopol wakiwa wamebeba bendera za jeshi la wanawamaji la Urusi.

 

Kenya: Wajumbe wa ODM wazua vurugu

Vurugu zimezuka katika uchaguzi wa kuwachagua maafisa wapya wa chama kikuu cha upinzani cha ODM nchini Kenya, chake aliyekuwa waziri mkuu wa taifa hilo Raila Odinga.

 

Bwana Odinga anatarajiwa na wengi kuwa atagombea kiti cha urais 2017

 Polisi waliwasili katika ukumbi wa uwanja wa michezo wa kimataifa wa Kasarani viungani mwa jiji la Nairobi kurejesha utulivu baada ya baadhi ya wafuasi wa chama hicho waliodaiwa kuwa walinda usalama kurusha vita pamoja na masanduku ya kupigia kura wakijaribu kuvuruga uchaguzi huo.

Ugomvi ulizuka baada ya kuzuka madai kuwa kulikuwa na orodha ya wajumbe bandia iliyokuwa ikisambazwa pamoja na makaratasi bandia ya kupigia kura. Mbunge maalum Isaac Mwaura ambaye anaishi na ulemavu wa ngozi-Albino-alionekana akisukwasukwa na wajumbe baada ya kuzua zahama kuhusu madai hayo ya udanganyifu katika zoezi hilo la upigaji kura.
Chama cha ODM ndicho chama kikubwa zaidi cha kisiasa nchini Kenya kikiwa na idadi kubwa ya wabunge katika bunge la kitaifa pamoja na Senate. Chama hicho kimemudu mgao mkubwa zaidi wa pesa za kufadhili shughuli za vyama vya kisiasa kutoka kwa serikali ya Kenya.
Kutokana na raslimali za chama hicho uchaguzi wa leo umeonekana kuzua msisimko mkali pamoja na patashika baina ya wanasiasa mashuhuru ambao wanagombania vyeo mbali mbali.
Bwana Odinga ambaye alishindwa na rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu uliokumbwa na madai ya udanganyifu mwezi Machi mwaka uliopita anatetea kiti chake kama kiongozi wa chama, dalili kwamba huenda akagombea tena kiti cha urais mwaka 2017.
Akizungumza kabla ya kuanza kwa zoezi la upigaji kura Bwana Odinga alizungumzia maswala mbali mbali yanayohusiana na usalama nchini Kenya pamoja na kuiponda serikali ya mpinzani wake Rais Uhuru Kenyatta kwa kushindwa kuleta suluhu ya matatizo ya kiuchumi yanayowakabili wakenya.

 

Shambulizi lawaua 12 Mogadishu

Mshambuliaji wa kujitoa muhanga amejilipua ndani ya gari na kuwauwa watu 12 na kujeruhi wengine wanane mjini Mogadishu Somalia.

 

Mogadishu imeshuhudia mashambulizi ya mara kwa mara hivi karibuni

Mlipuko huo umetokea nje ya makao makuu ya maafisa wa usalama .
Mwandishi wa BBC anasema kuwa waliofariki ni maafisa usalama na wengine raia wa kawaida waliokuwa katika mkahawa karibu na hapo.
Kumekuwa na ongezeko la mashambulizi huku vikosi vya nchi hiyo vikipambana na wanamgambo wa al shaabab.
Kundi la wanamgambo la Al Shabaab limekiri kufanya shambulizi hilo ambalo limetokea chini ya wiki mbili baada ya kundi hilo kushambulia ikulu ya Rais mjini Mogadishu
Msemaji wa kijeshi wa kundi hilo amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema kuwa huu ndio mwanzo tu wa kundi hilo kushambulia Mogadishu na kwamba operesheni yao itaendelea.
Alisema kuwa shambulio hilo lililenga maafisa wa usalama waliokuwa wameketi katika mkahawa mmoja na kuwaua watu 11 huku 15 wakijeruhiwa.

 

Marekani kuleta umeme Afrika

Wabunge nchini marekani wameidhinisha mpango wa kuleta umeme kwa zaidi ya watu millioni hamsini katika jangwa la Sahara barani Afrika na hivyo basi kutoa fursa kwa mradi huo wa serikali ya Obama kuanza kutekelezwa.

      

Mswada huo uliopitishwa na kamati ya maswala ya kigeni nchini humo unalenga kujenga megawati elfu ishirini barani Afrika ifikiapo mwaka 2020 na kuwafikia watu elfu hamsini ambao wanaishi bila umeme.

Mpango huo ulitangazwa na rais Obama wakati wa ziara yake barani afrika mnamo mwezi juni mwaka jana.
Mswada huo utahitajika kupitishwa na bunge la wawakilishi pamoja na lile la sineti lakini hatua hiyo ya kamati ya maswala ya kigeni ni dhihirisho tosha kwamba unuangwa mkono na pande zote za kisiasa.

 

Wanafunzi wa Tanzania Thailand Waizungumzia sekta ya Madini.

                    

1 
Kamishna Msaidizi wa Madini  Mhandisi Hamis Komba katikati akiwa pamoja na Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma masomo ya Geomolojia katika Chuo cha ‘Asian Institute of Geological Science’ (AIGS) nchini Thailand. Wa kwanza kulia ni Agatha Mwinuka, anayefuata ni Emmanuel Minja na wa kwanza 

kushoto ni Doricas Moshi. Wanafunzi wa Kitanzania nchini Thailand, wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wenzao kutoka mataifa mbalimbali , ambao wamelitembelea  banda la Tanzania.
   
Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini katika picha ya pamoja na wanafunzi hao katika banda la Tanzania.
2
3 (2)
……………………………………………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Bangkok
Wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma masomo ya Geomolojia katika Chuo cha ‘Asian Institute of Geological Science’ (AIGS) nchini Thailand, wamewataka wadau wa tasnia ya madini ya vito na usonara nchini Tanzania kuichukua sekta hiyo kwa umakini mkubwa kutokana na  mchango wake kiuchumi.
Aidha, wameeleza kuwa, nchi ya Thailand imepiga hatua kubwa katika sekta ya madini ukilinganisha na Tanzania lakini bado Tanzania inaweza kufaidika zaidi katika sekta hiyo ikiwa kila mdau atatimiza wajibu wake kikamilifu ili madini ya vito yaongeze mchango katika pato la taifa.
Wameongeza kuwa, Tanzania bado ina nafasi ya kujipanga upya kuhusu kuboresha zaidi sekta hiyo kama ilivyo kwa nchi nyingine  endapo mipango mikakati ya maboresho itatekelezwa  na kusimamiwa kikamilifu.
Wanafunzi hao wameyasema hayo, wakati walipolitembelea banda la Tanzania katika maonesho ya 53 ya Vito vya Usonara na Madini yanayoendelea katika jiji la Bangkok ambapo nchi zaidi ya 150 zinashiriki maonesho hayo.
“Thailand wamejipanga vizuri katika sekta ya madini. Wafanyabiashara wa madini wana umoja. Wadau wa madini wanatakiwa kuelewa  kuwa madini yanawakilisha utajiri wetu tulionao”. Amesema Agatha Mwinuka.
Aidha, wameitaka serikali na  wadau wa Tanzania  wanaoshiriki maonesho hayo kujifunza kutokana na changamoto wanazozipata kutoka kwa nchi nyingine, jambo ambalo litasaidia kuboresha sekta ya madini na vito, ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara kuhakikisha  kuwa wanafuata sheria na taratibu zilizopo.
“Tunaiomba serikali iendelee kuendeleza viwanda vya kukata madini. Ni jambo zuri kama shughuli hizi za kukata madini zitafanyika ndani ya nchi badala ya nje. Jambo hili linasaidia sana kuongeza thamani ya madini.  Ameongeza, Emmanuel Minja.
Akiongelea kuhusu umuhimu wa kuendeleza na kuboresha kituo cha Tanzania Geomological Center,  Doricas Moshi, ameeleza kuwa,  kituo hicho kinaweza kutoa mchango mkubwa katika tasnia hii hasa katika nyanja ya ukataji madini  na uthamini wa madini hivyo, ameitaka Serikali kukiongezea nguvu kituo hicho kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo ya  Tanzania.
“Chuotunachosoma hapa kinatumia sana mifano ya madini ya Tanzania katika kufundisha.  Mengi yametoka nyumbani, hii ni ishara nzuri. Serikali iliangalie hili. Ameongeza Doricas.
Aidha, wameeleza kuwa, soko la kimataifa kwa madini ya Tanzania lipo, hivyo, wamewataka wadau wote kuhakikisha wanashirikiana vizuri na serikali kuendeleza sekta hiyo kutokana na umuhimu na mchango wake kwa taifa. 
Akizungumzia  mipango iliyopo ya kuboresha sekta hiyo, Kamishna Msaidizi wa Madini, Mhandisi Hamis Komba, amesema kuwa, Serikali kupitia Shirika la Madini Tanzania (STAMICO), inatekeleza mikakati ya kuwasaidia wachimbaji wadogo na wa kati  ili waweze kuendana na   mahitaji ya soko la kimataifa kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali yakiwemo ya kukata madini, kuyaongezea thamani na  kuwapatia mikopo kupitia Benki ya TIB.
“STAMICO imepewa jukumu la kuwaendeleza wachimbaji wadogo katika sekta ya madini hususani katika masuala ya uchimbaji, uongezaji thamani madini na biashara ya madini. Serikali imejipanga vizuri katika hilo”. Ameongeza Kamishana. 
Ameongeza kuwa, Serikali inatambua kwamba wachimbaji wengi wapo katika sekta ya madini ya vito na usonara hivyo, jitihada za kuwaendeleza  zitasaidia kufikia kiwango bora cha utendaji wao wa kazi.
Vilevile, ameongeza kuwa, kutokana na kuboreshwa kwa Sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo inaiwezesha STAMICO kumiliki asilimia 50 ya hisa katika mgodi wa Tanzanite One, jambo ambalo linaifanya Serikali kuwa mmiliki katika mgodi huo