MADEREVA WA MALORI
ZAIDI YA 300 WAGOMA KUENDELEA NA SAFARI KATIKA BARABARA KUU ITOKAYO
DODOMA HADI MWANZA BAADA YA MWENZAO KUVAMIWA
Madereva wa malori zaidi ya mia tatu wamegoma kuendelea na safari katika
barabara kuu itokayo Dodoma hadi Mwanza baada ya dereva mwezao
aliyekuwa akiendesha lori kuvamiwa na majambazi katika eneo la kisaki
manispaa ya Singida.
Wakiongea na ITV /Radio one madereva ambao wamekutwa katika eneo hilo
wameomba jeshi la polisi kufanya doria mara kwa mara eneo hilo kwani
kumekuwa na matuki yanayo jirudia ya utekeji wa magari kwa kuweka mawe
makubwa barabarani na kuwajeruhi madereva jambo ambalo lina tishia
amani kwa watumiaji wa barabara.
Madereva wa malori baada ya
kufunga barabara naibu waziri wa Afrika mashariki Dr. Abdulla Abdulla
alikumbwa na adha hiyo na kusema ni haki ya kikatiba kwa madereva kugoma
kwa kudai haki zao, kutokana na hali hiyo amewahaidi madereva kupeleka
kilio chao katika mamlaka husika ili kuweza kutatua tatizo lao na
kukomesha vitendo vya uvamizi wa magari katika eneo hilo .
Kwa
upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida SACP Geofrey
Kamwela amesema madereva waliamua kusimama barabarani bila sababu yeyote
kwa muda wa zaidi ya masaa matatu na kusababisha foleni kubwa ambapo
kwamujibu wa sheria za usalama barabarani walikuwa wamefanya kosa
,lakini baada ya viongozi kufika na kuwasikiliza waliamua kuendelea na
safari.
Naye dereva wa lori bwana Agustino Mbawala aliye tekwa,
akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida akiongea kwa shida
huku akiwa na maumivu makali amesema aliona mawe makubwa barabarani na
kuamua kusimama na kukimbia lakini wali mvamia na kumpiga hatimaye
kumpora fedha na simu
No comments:
Post a Comment