Monday, 24 March 2014

Marekani kusaidia UG kupambana na Kony


Kiongozi wa waasi wa LRA Joseph Kony

 Serikali ya Marekani inatuma ndege ya kivita na kikosii maalum cha jeshi kusaidia Uganda katika juhudi za kumsaka kiongozi wa kundi la waasi la Lord's Resistance Army, Joseph Kony.Msemaji wa baraza la usalama la Marekani, Caitlin Hayden, amesema kuwa wanajeshi wa Afrika wataendelea kuongoza operesheni hiyo, ingawa watapata ushauri kutoka kwa vikosi vya Marekani.Alisema kuwa ndege hiyo itawekwa nchini Uganda ingawa itatumika katika nchi zingine ambako waasi wa LRA wamekuwa wakijificha.Marekani ilituma vikosi vyake mara ya kwanza nchini Uganda mwaka 2011 kusaidia Uganda katika harakati za kumtafuta Joseph Kony.

 

529 wahukumiwa kifo Misri

Mahakama nchini Misri imewahukumu kifo watu 529 ambao wanasemekana kuwa wafuasi wa Rais aliyeng'olewa mamlakani Mohammed Morsi.
Watu hao walikabiliwa ma mashitika mbali mbali yakiwemo mauaji ya polisi na kuwavamia polisi.
Wafuasi hao wa chama kilichopigwa marufuku, cha Muslim Brotherhood, ni sehemu ya kundi lengine kubwa la watu zaidi ya 1,200 wanaoaminika kuwa wafuasi wa Morsi.
Maafisa wa utawala nchini Misri wamekuwa wakiendesha msako mkubwa dhidi ya wafuasi wa vuguvugu hilo, tangu Morsi kuondolewa mamlakani mwezi Julai mwaka jana.
Maelfu wamekamatwa huku mamia wakiuawa.
Mahakama hiyo ilitoa hukumu baada ya vikao viwili pekee ambapo mawakili wa watuhumiwa walilalamika kuwa hawakupewa muda wa kuwasilisha kesi yao vyema.
Mauaji wanayodaiwa kufanywa na watuhumiwa yalitokea Kusini mwa Misri, mwezi Agosti, baada ya vikosi vya usalama kuvunja kambi mbili za wafuasi wa Morsi waliokuwa wanataka arejeshwe mamlakani

 

Makahaba watumia Vibaya Hijab Kenya

Makahaba katika baadhi ya sehemu za mji mkuu wa Kenya , Nairobi, wametupilia Mbali vazi la 'Mini skirt na kuanza kutumia Hijab kama njia ya kuwavutia wateja wao, jambo ambalo limekashifiwa vikali na wakuu wa dini ya Kiislamu.
Hijab huvaliwa na wanawake wa Kiislamu kama ishara ya kumcha Mungu, lakini makahaba katika mtaa wa Eastleigh, viungani mwa Nairobi wanatumia Hijab ili kuwafanya wateja wao kudhania kua wanatoka sehemu za Pwani.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa mtandao wa shirika la habari la Nation mjini Nairobi.
Mwanamke mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema kuwa yeye hupata wateja maradufu kwani huvalia vazi hilo la Hijab, wengi wa wateja wake wakimuona kama mwenye nidhamu.
Uchunguzi ulibaini kuwa wanawake wasio wa kiislamu wanavalia vazi hilo ili kuwavutia wanaume ambao wanaamini kuwa wao wana maadili zaidi ya wale wanaovalia nguo fupi au 'Mini Skirt'.
Nguo fupi ni mavazi yaliyozoeleka kwa makahaba sehemu nyingi duniani
Taarifa hiyo imemnukuu Imam mkuu wa msikiti wa Jamia mjini Nairobi, Mohamed Swalihu akisema kuwa ni jambo la kusikitisha sana kuwa Hijab inatumika kwa njia isiyopaswa na makahaba huku akiongeza kuwa pia wanaume wanalitumia vazi hilo kuendesha shughuli za uhalifu jambo ambalo amelitaja kuwa la kishetani linalostahili kukashifiwa vikali.
Hata hivyo chama cha makahaba nchini Kenya kimewatetea makahaba hao wanaotumia hijab huku likidai kwamba wanafanya hivyo ili kukidhi mahitaji ya wateja wao.
Mratibu wa muungano huo, Bi Phelister Abdalla, aliiomba serikali kuhalalisha ukahaba kwa madai ya viwango vya juu vya ukosefu wa ajira.
Mahojiano na makahaba katika mtaa wa Eastleigh yalibaini kwamba wanaume hawakuwa na haja ya wanawake wenye kuvalia nguo fupi badala yake wakipendelea wanawake wa kiislamu na wale wa kutoka Ethiopia.

Monday, 17 March 2014


RIDHIWANI AANZA MBIO ZA KUSAKA KURA JIMBO LA CHALINZE‏


Meneja wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Steven Kazidi (kushoto) akimuinua mkono juu kwa ishara ya kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo (CCM), Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa mkutano wa kwanza wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Matipwili, Saadani Wilayani Bagamoyo jana Machi 14,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM), Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Matipwili, Saadani Wilayani Bagamoyo, wakati wa mkutano wa kwanza wa kampeni zake ulioanza rasmi jana Machi 14,2014.Baada ya kumaliza Mkutano na Wananchi wa Kijiji cha Matipwili, Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ndg. Ridhiwani Jakaya Kikwete alifika katika Kijiji cha Gongo ndani ya Tarafa ya Saadani na kukutana na wananchi wa Kijiji hicho na kuzungumza nao kama aonekanavyo pichani.

Mbunge wa Arumeru Mshariki , Joshua Nassari aumbuka bungeni




Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Joshua Nassari, juzi alijikuta akiumbuka bungeni baada ya kushindwa kutaja kanuni aliyoitumia, kuomba mwongozo. 
 
Hali hiyo ilitokea muda mfupi kabla ya wajumbe kupiga kura za kumchagua Mwenyekiti wa Bunge hilo.
 
Kuumbuka kwa mjumbe huyo ambaye pia ni Mbunge wa Arumeru Mshariki, kulitokana na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho, kumtaka kutaja kanuni aliyoitumia.
 
Hata hivyo, baada ya kusita kwa muda Nassari bila kutaja kanuni aliyoitumia, alisema wajumbe wengi hawajasikia utaratibu unaotumika katika upigaji kura kwa sababu walichelewa kwenye msongamano wa watu getini.
 
“Wengi wetu tumeingia tukiwa tumechelewa kwa sababu wengi tunapita katika geti moja. Ningependa ufafanuzi wako kuhusu aina ya kura tunayokwenda kupiga ni ya wazi au ya siri,”alisema.
 
Hata hivyo, kificho alimjibu kuwa kura zitakazopigwa kumchagua mwenyekiti zitakuwa ni za siri.
 
Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya Bunge hilo kupitisha kanuni za uendeshaji wake ambapo hata hivyo nyingine bado zimekuwa na mgongano wa maridhiano kwa baadhi ya wajumbe kutaka ufafanuzi zaidi.

Tuesday, 11 March 2014

GARI LA KUBEBEA TAKA LILILOACHWA KITUO CHA GEREJI BARABARA YA MANDELA LAWA KERO KWA ABIRIA WANAOTUMIA KITUO HICHO 

 

 

Lori la kubeba taka likiwa eneo kituo cha gereji barabara ya mandela road,huku likiwa limebeba uchafu baada ya kuharibika na limekaa hapo siku mbili.

 

Huo unaonekana kwa juu ni uchafu uliooza na unatoa harufu kali kituoni hapo. eneo la kituo cha gereji mandela road 

 

Abiria wanaotumia kituo cha gereji barabara ya mandela kwa siku mbili mfululizo wamekuwa wakipata kero ya harufu kali inayosababishwa na gari ya kubebea taka iliyopaki kwenye kituo hiko.Wakiongea na mtandao wa wetu huu wa Dj sek abiria hao wamesema kwamba gari hiyo iliharibika ikiwa inaelekea kumwaga uchafu huo na wakaisogeza kituoni hapo ili waweze kuitengeneza, lakini badala yake dereva na wasaidizi wake wakaitelekeza gari iyo toka juzi.Wakiendeleaa kuongea na mtandao wetu wamesema eneo lote la kituoni hapo linatoa harufu kali ambayo ni kero kwa wao wanaosubilia usafiri eneo hilo.

Mwandishi wa blog hii nilishuhudia mwenyewe na kupiga picha pia kuonja adha ya harufu kali inayotoka kwenye gari hiyo.Manispaa ya kinondoni na wasimamizi wa usafi mnaombwa kufuatilia hili na kuweza kulitatua kwani ni kero kwa watumiaji wa kituo hiki. 

KAMPUNI YA GOOGLE YAKANUSHA PICHA YA GOOGLE MAP INAYOONESHA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA 

KAMPUNI YA GOOGLE YAKANUSHA PICHA YA GOOGLE MAP INAYOONESHA NDEGE YA MALAYSIA ILIYOPOTEA

Kampuni ya google imekanusha habari zilizotapakaa kwenye mitandao mbalimbali duniani kwa kuweka picha ya Google Map ambayo inaonesha ndege ya Malaysia Airline ikiwa imedondondoka ndani ya maji. Msemaji wa google nchini Malaysia amesema
"Yes, the images may be there, but it is not real time satellite images as the images may have provided to us several weeks or months ago," he said when contacted.
Hii imetokana na kutapakaa kwa picha inayoonesha ndege ya Malaysia Airline imedondoka kwenye maji.
Mpaka sasa meli zipatazo 40 na ndege 34 zinazunguka bahari inayizunguka maeneo ya Vietnam na Malysia wakitafuta ndege ya Malaysia Airline iliyopotea toka jumamosi.
Nchi zinazoshiriki kuitafuta ndege hiyo ni Australia, China, Thailand, Indonesia, Singapore, Vietnam, Philippines, New Zealand na Marekani.