Friday, 1 August 2014
Wema Sepetu na Martin Kadinda wamekuwa karibu sana hasa ukizingatia kuwa Kadinda amekuwa manager wa Wema kwa muda mrefu.Hizi ni picha alizo share Wema siku za nyuma ila hadi leo zimekuwa zina make headline kwenye mtandao wa Instagram.
Baada ya Wema kueleza alivyo m-miss, Hizi ndizo picha alizo share Ommy Dimpoz akiwa na Wema
Siku tano zilizo pita kupitia mtandao wa Instagram, Mwigizaji wa filamu hapa Tanzania, Wema Sepetu aliandika kuwa ame mmiss msanii wa nyimbo za bongo fleava Ommy Dimpoz.Huyu binadamu jamani tokea nimuone kwenye Mtv Awards sijamuona mpaka leo... Kiukweli nimemmiss saaaaana.... Mpuuzi wangu mwenyewe... Miss u shem lake... @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz
Haya ndiyo majibu ya Ommy Dimpoz ambapo ame share picha wakiwa pamoja na Wema Sepetu.
Monday, 19 May 2014
5 wauawa katika mlipuko Nigeria
Bomu lililolipuka katika mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria limewaua watu 5 na kuwajeruhi wengine wengi.
Shambulio hilo limefanywa katika eneo
linaloaminiwa kuwa na waumini wengi zaidi wa dini ya kikristu, ambao
wamekuwa wakilengwa mara nyingi na wapiganaji wa Boko Haram.Mwandishi wa BBC mjini Abuja Will Ross anasema kuwa eneo hilo lililolengwa linajulikana kama Sabon Gari. Watu wengi walikuwa kwenye migahawa ya vileo na kwenye barabara. Amesema kuwa kilichosalia kwenye gari lililokuwa na bomu hiyo ni injini pekee.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja mji wa Kano umepumzika kutokana na mashambulio, hasa kwasababu ya oparesheni kali iliyofanywa na maafisa wa usalama kuwasaka wanamgambo hao wa Boko Haram.
Mlipuko wa bomu Nigeria
Mashambulio ya awali
Mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kituo cha basi kilishambuliwa kwa bomu na awali mwaka wa 2012, Boko Haram walifanya shambulio baya zaidi lililowaua zaidi ya watu 150 katika msururu wa milipuko.Kundi hilo bado linawazuilia wasichana zaidi ya 200 wa shule, lililowateka kutoka kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa Nigeria mwezi mmoja uliopita.
Nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Ufaransa na Marekani wameahidi kutuma wanajeshi kusaidia kuwakomboa wasichana hao.
Nao viongozi wa Afrika wanaokutana mjini Paris wametangaza 'vita' dhidi ya Boko Haram na kuahidi kushirikiana ki-intelijensia na kijeshi, kupambana na Boko Haram.
Wednesday, 7 May 2014
Rais Kikwete afungua mkutano wa Majaji Wanawake Arusha
Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete,Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Asha Rose Migiro,Jaji Mkuu
Mohamed Othman Chande,pamoja na Rais wa Chama Cha Kimataifa cha Majaji
Wanawake wakiimba wimbo wa taifa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 12 wa
chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha
AICC.Mkutano huo ulifunguliwa na Rais Kikwete.
Baadhi ya majaji wanawake
wanaoshiriki Mkutano wa 12 wa Chama Cha Kimataifa cha Majaji wanawake
unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano mjini ArushaTANKI LA MAFUTA LALIPUKA NA KUSABABISHA ADHA KUBWA KWA WASAFIRI MAENEO YA SHELUI SINGIDA
Baadhi
ya wananchi wakipiga picha wakati tanki la mafuta la kampuni ya B.
Clarke Haulege Construction, Tanki hilo ni mali ya Bw. Bundala Kapela wa
Igunga ni namba T634 BCZ lenye vyumba vinne na uwezo wa kubeba lita
40.000 za mafuta ya Petroli lililipuka majira ya Saa 11:00 katika
barabara kuu ya Dodoma Mwanza eneo la Shelui mkoani Singida wakati breki
za tanki hilo upande wa kushoto zilipojam na kusababisha moto, Jambo
lililomfanya dereva wa roli lenye namba za usajiri T 164 CGF aina ya
Scania lililokuwa likivuta tanki hilo kusimamisha
na kukata haraka tanki hilo huku akiondoa haraka injini ili kuepusha
madhara zaidi ambayo yangeweza kutokea, Katika tukio hilo
lililosababisha usumbufu mkubwa kwa abiria na msururu wa magari
kushindwa kupita kutokana na moto mkubwa uliochanganyika na moshi
kutishia usalama wa watumiaji wengine, hata hivyo baada ya moto
kupungua kiasi askari wa usalama barabarani waliamuru magari yaanze
kupitia pembeni mwa barabara hiyo ili kuendelea na safari, Hakuna mtu
aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo, Angalia matukio
zaidi ya picha hapo chini. (PICHA NA FULLSHANGWE)
Msururu wa magari ukiwa mkubwa katika eneo hilo baada ya kushindwa kupita kutokana na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka. 
Askari wa usalama barabarani akihakikisha mambo yanakwenda sawana usalama unaimarishwa katika eneo hilo.
Airtel yazindua duka la kisasa Mlimani City
Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet akikata utepe kuzindua
duka la Airtel lililopo mlimani city jijini Dar es Saalam.wakishuhidia,
wapili ni Andre Beyers Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika akiwa na meneja
wa duka Wahida Saleh na Sunil Colaso Mkurugenzi Mkuu Airtel Tanzania
duka la Airtel lililopo mlimani city jijini Dar es Saalam.wakishuhidia,
wapili ni Andre Beyers Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika akiwa na meneja
wa duka Wahida Saleh na Sunil Colaso Mkurugenzi Mkuu Airtel Tanzania
Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet akikata utepe kuzindua
duka la Airtel lililopo mlimani city jijini Dar es Saalam.wakishuhidia,
wapili ni Andre Beyers Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika akiwa na meneja
wa duka Wahida Saleh na Adriana Lyamba Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa
wateja Airtel Tanzaania
duka la Airtel lililopo mlimani city jijini Dar es Saalam.wakishuhidia,
wapili ni Andre Beyers Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika akiwa na meneja
wa duka Wahida Saleh na Adriana Lyamba Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa
wateja Airtel Tanzaania
Saturday, 12 April 2014
JINSI MAFURIKO YANAVYOLITESA JIJI LA DAR..ANGALIA PICHA
Subscribe to:
Posts (Atom)