Tuesday, 5 August 2014



ALIKIB AFUNGUKA KUHUSU LULU. AONGELEA PIA TUHUMA ZA KUMTOA BIKRA JACKLINE WOLPER

HII ni exclusive! Kwa mara ya kwanza, staa anayeitikisa nchi kwa sasa na wimbo wake wa Mwana, Ali Kiba amefunguka kuwa mwigizaji kiwango Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ anafaa kuwa mke (wife material) huku akiweka wazi sifa kibao alizonazo, Wikienda liko bize kukujuza.
Staa anayeitikisa nchi kwa sasa na wimbo wake wa Mwana, Ali Kiba ndani ya ofisi za global.
Kiba ambaye hivi karibuni ameibua mijadala mingi katika mitandao ya kijamii, usafiri wa umma na kwenye baa juu ya ujio wake mpya akisemekana kurudia kiti chake ambacho alikikalia Mbongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond’ kwa muda, mwaka 2010 aliwahi kuripotiwa katika magazeti pendwa kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na Lulu ambaye wakati huo alikuwa na umri chini ya miaka 18!
LULU ANAFAA KUWA MKE
Akizungumza mbele ya kinasa sauti cha Globa TV Online, Bamaga-Mwenge jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Kiba ambaye anatarajia kuangusha shoo ya kihistoria Agosti 8, mwaka huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, alisema Lulu anafaa kuwa mke kwa vile ni mchapakazi sifa ambayo mke mwema anapaswa kuwa nayo.
AMMWAGIA SIFA
Kiba alisema Lulu anajua kuhangaika, anajua kupambana kusaka pato lake kihalali kupitia mauzo ya sinema zake anazozizalisha kitu ambacho kinawashinda mabinti wengi na kuangukia katika biashara ya kuuza miili (ukahaba).
Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ akiwa na Ali Kiba.
Licha ya kummwagia sifa hizo, kipindi hicho alichokuwa akitajwa kuwa naye, Lulu alikuwa na matukio ambayo hayakuwa na maadili lakini Kiba hayo hakuyatilia maanani.
Mwandishi: Unafikiri Lulu ni ‘wife material’ (mke mwema) ambaye unaweza kumweka ndani akalea watoto na kuijenga familia bora?
Kiba: Yeah! Anafaa kuwa mke, ni binti anayejituma, mchapakazi, mtafutaji. Kwangu mimi mtu wa namna hiyo ndiyo anafaa kuwa mke.
Mwandishi: So, unataka kutuambia kwamba unaweza kumuoa?
Kiba: Sijasema hivyo mimi, nimesema anafaa kuwa mke.
ACHOMOA KUBANWA KISHERIA
Licha ya kuchomoa ishu hiyo ya uhusiano, mapaparazi wetu walimbana zaidi staa huyo afafanue kwa nini alitajwa yeye na si msanii mwingine huku ikidaiwa kuwa, Lulu hakuwa ametimiza miaka 18 hivyo kubanwa kisheria (ya watoto na kujamiiana).
“Sijatembea naye ndiyo maana unaona hata sheria haijanihukumu, endapo ningekuwa nimetembea naye, basi sheria ingeweza kunitia hatiani na ningefungwa jela,” alifafanua Kiba.
  'Kanumba The Great' enzi za uhaim wake.
AWASHANGAA WANAOMSHANGAA
Kiba aliongeza kuwa, anashangaa sana kuona watu wanamsema vibaya yeye kupendwa na Lulu.
“Lulu ni msanii mwenzangu, anapenda kazi zangu na mimi napenda za kwake. Ni rafiki wa kawaida, hakuna kitu kingine cha ziada. Nawashangaa wanaozusha ya kuzusha, hivi kwani kuna tatizo Lulu akinipenda? Sidhani kama ni kosa, ana haki ya kunipenda kutokana na muziki wangu.
“Unajua muziki mzuri huwa unapenya automatically, huwezi kuzuia hisia za muziki, mtu unaweza ukawa humpendi msanii f’lani lakini ukapenda muziki wake, unajikuta tu unampenda, unaanza kuimba nyimbo zake,” alisema Kiba.
KUMBUKUMBU MBICHI
Juzikati wakati Kiba anatambulisha nyimbo zake mbili kwa mpigo (Mwana na Kimasomaso), Lulu, kupitia mtandao wa Instagram alitupia maneno ya kummwagia sifa staa huyo, liliibuka kundi ambalo linatajwa kuwa ni wafuasi wa mwigizaji Wema Sepetu ‘Team Wema’ na kuanza kumshambulia kwa maneno machafu.
KIBA AFUNGUKA
Akizungumzia ishu hiyo, Kiba alisema waliofanya hivyo hawakumtendea haki Lulu kwani ana haki ya kueleza hisia zake pale anapoguswa na muziki mzuri.
“Hawajatenda haki kwa sababu Lulu ni binadamu kama walivyo wengine, ana haki ya kupenda kitu kizuri,” alisema Kiba.
KUHUSU KIFO CHA KANUMBA
Kiba akizungumzia juu ya kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa nyota wa sinema Bongo, marehemu Steven Kanumba ambapo alidaiwa kunaswa kwa meseji za mapenzi alizozituma kwa Lulu ndiyo zilizosababisha mtifuano ambao ulisababisha kifo cha Kanumba, alikana madai hayo.
“Si kweli, sikuwa nimewasiliana na Lulu siku hiyo kabla ya tukio. Nakumbuka nilikuwa safarini, baada ya tukio nilimpigia Lulu kutaka kujua ukweli wa taarifa za kifo kwa sababu marehemu alikuwa mtu wangu  wa karibu kama alivyo Lulu,” alisema Kiba.
AMGUSIA WOLPER
Kwenye mahojiano hayo, mkali huyo alizungumzia ishu ya mwigizaji, Jacqueline Wolper kukiri kwamba Kiba ndiye mwanaume aliyemtoa usichana wake kwenye simulizi iliyochapishwa katika Gazeti la Championi hivi karibuni.
“Mh! Aliwahi kukiri? Daah! Sijui bwana… Wolper ni mtu wangu wa karibu kama alivyo Lulu,” alisema kwa mkato Kiba.Juzi, Lulu alitafutwa na mapaparazi wetu ili  azungumzie ukaribu wake na Kiba, lakini simu yake muda mwingi iliita bila kupokelewa (tunaamini atasoma hapa, tunaendelea kumtafuta ili afunguke).
Ili kupata mahojiano hayo kwa kirefu zaidi, fuatilia tovuti ya

Friday, 1 August 2014

Picha hizi za Wema Sepetu na Martin Kadinda zina make headline kutizamwa kwenye mitandao 

Wema Sepetu na Martin Kadinda wamekuwa karibu sana hasa ukizingatia kuwa Kadinda amekuwa manager wa Wema kwa muda mrefu.Hizi ni picha alizo share Wema siku za nyuma ila hadi leo zimekuwa zina make headline kwenye mtandao wa Instagram.

  

Baada ya Wema kueleza alivyo m-miss, Hizi ndizo picha alizo share Ommy Dimpoz akiwa na Wema 

Siku tano zilizo pita kupitia mtandao wa Instagram, Mwigizaji wa filamu hapa Tanzania, Wema Sepetu aliandika kuwa ame mmiss msanii wa nyimbo za bongo fleava Ommy Dimpoz.
Huyu binadamu jamani tokea nimuone kwenye Mtv Awards sijamuona mpaka leo... Kiukweli nimemmiss saaaaana.... Mpuuzi wangu mwenyewe... Miss u shem lake... @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz

Haya ndiyo majibu ya Ommy Dimpoz ambapo ame share picha wakiwa pamoja na Wema Sepetu.


 

Monday, 19 May 2014

5 wauawa katika mlipuko Nigeria

Bomu lililolipuka katika mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria limewaua watu 5 na kuwajeruhi wengine wengi.
Shambulio hilo limefanywa katika eneo linaloaminiwa kuwa na waumini wengi zaidi wa dini ya kikristu, ambao wamekuwa wakilengwa mara nyingi na wapiganaji wa Boko Haram.
Mwandishi wa BBC mjini Abuja Will Ross anasema kuwa eneo hilo lililolengwa linajulikana kama Sabon Gari. Watu wengi walikuwa kwenye migahawa ya vileo na kwenye barabara. Amesema kuwa kilichosalia kwenye gari lililokuwa na bomu hiyo ni injini pekee.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja mji wa Kano umepumzika kutokana na mashambulio, hasa kwasababu ya oparesheni kali iliyofanywa na maafisa wa usalama kuwasaka wanamgambo hao wa Boko Haram.


Mlipuko wa bomu Nigeria 

Mashambulio ya awali

Mnamo mwezi Machi mwaka uliopita kituo cha basi kilishambuliwa kwa bomu na awali mwaka wa 2012, Boko Haram walifanya shambulio baya zaidi lililowaua zaidi ya watu 150 katika msururu wa milipuko.
Kundi hilo bado linawazuilia wasichana zaidi ya 200 wa shule, lililowateka kutoka kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa Nigeria mwezi mmoja uliopita.
Nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Ufaransa na Marekani wameahidi kutuma wanajeshi kusaidia kuwakomboa wasichana hao.
Nao viongozi wa Afrika wanaokutana mjini Paris wametangaza 'vita' dhidi ya Boko Haram na kuahidi kushirikiana ki-intelijensia na kijeshi, kupambana na Boko Haram.


 

Wednesday, 7 May 2014

Rais Kikwete afungua mkutano wa Majaji Wanawake Arusha

      
mpya 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Asha Rose Migiro,Jaji Mkuu Mohamed Othman Chande,pamoja na Rais wa Chama Cha Kimataifa cha Majaji Wanawake wakiimba wimbo wa taifa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 12 wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha AICC.Mkutano huo ulifunguliwa na Rais Kikwete.22bh nhnmhjm
Baadhi ya majaji wanawake wanaoshiriki Mkutano wa 12 wa Chama Cha Kimataifa cha Majaji  wanawake unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano mjini Arusha

TANKI LA MAFUTA LALIPUKA NA KUSABABISHA ADHA KUBWA KWA WASAFIRI MAENEO YA SHELUI SINGIDA

       
7
Baadhi ya wananchi wakipiga picha wakati tanki la mafuta la kampuni ya B. Clarke Haulege Construction, Tanki hilo ni mali ya Bw. Bundala Kapela wa Igunga ni namba T634 BCZ lenye vyumba vinne na uwezo wa kubeba lita 40.000 za mafuta ya Petroli lililipuka majira ya Saa 11:00 katika barabara kuu ya Dodoma Mwanza eneo la Shelui mkoani Singida wakati breki za tanki hilo upande wa kushoto zilipojam na kusababisha moto, Jambo lililomfanya dereva wa roli lenye namba za usajiri T 164 CGF aina ya Scania lililokuwa likivuta tanki hilo kusimamisha na kukata haraka tanki hilo huku akiondoa haraka injini ili kuepusha madhara zaidi ambayo yangeweza kutokea, Katika tukio hilo lililosababisha usumbufu mkubwa kwa abiria  na msururu wa magari kushindwa kupita  kutokana na moto mkubwa uliochanganyika na moshi kutishia usalama wa watumiaji wengine, hata hivyo  baada ya moto kupungua kiasi askari wa usalama barabarani waliamuru magari yaanze kupitia pembeni mwa barabara hiyo ili kuendelea na safari, Hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo, Angalia matukio zaidi ya picha hapo chini. (PICHA NA FULLSHANGWE) 
 5 4 111
Msururu wa magari ukiwa mkubwa katika eneo hilo baada ya kushindwa kupita kutokana na moto mkubwa uliokuwa ukiwaka. 10
Wananchi na wasafiri mbalimbali wakitoka kuangalia tukio hilo. 8
Askari wa usalama barabarani akihakikisha mambo yanakwenda sawana usalama unaimarishwa katika eneo hilo.

Airtel yazindua duka la kisasa Mlimani City

      
pic 1a
Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet akikata utepe kuzindua
duka la  Airtel  lililopo mlimani city  jijini Dar es Saalam.wakishuhidia,
wapili ni Andre Beyers Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika akiwa na meneja
wa duka Wahida Saleh na Sunil Colaso Mkurugenzi Mkuu Airtel Tanzania
pic 1b
Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet akikata utepe kuzindua
duka la  Airtel  lililopo mlimani city  jijini Dar es Saalam.wakishuhidia,
wapili ni Andre Beyers Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika akiwa na meneja
wa duka Wahida Saleh na Adriana Lyamba Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa
wateja Airtel Tanzaania
pic 5b
Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet na  Afisa mkuu wa
masoko Airtel Afrika Andre Beyers wakiwa katika picha ya pmaoja na
wafanyakazi wa Airtel katika duka la mlimani City mara baada ya uzinduzi wa
duka hilo baada ya kufanyiwa matengenezo na kuwa la kisasa zaidi
pict 5
pic 10