Friday 28 February 2014

Tanzania tunapaswa kuiga hili: Roboti zatumika Kuongoza magari DRC

 

Roboti barabarani DRC

Je Roboti kubwa zenye sauti nzito na mikono mikubwa zinaweza kuwa jibu kwa kupunguza msongamano wa magari barabarani?
Hili ndilo suluhu abalo serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imebuni ili kupunguza foleni ya magari mjini Kinshasa.
Mbinu hii ya kupunguza foleni ya magari inafanyiwa majiribio mjini Kinshasa.
Roboti mbili zilizotengezwa na kikundi cha watu zimepata kuungwa mkono na wananchi na maafisa wakuu, wanasema kuwa zinasaidia kupunguza msongamano wa magari barabarani.
Mji wa Kinshasa una wakazi milioni 10 na sifa yake kuu ni uendeshaji ovyo wa magari pamoja na msongamano mkubwa wa magari.
Licha ya kuwepo roboti, kuna pia taa za kawaida ambazo hutumiwa kurahisisha kuelekeza magari barabarani. Magari makuu kuu na madereva wasiojali sana sheria za barabarani.
Polisi wa trafiki pia wamekuwa wakituhumiwa kwa kuchukua hongo kutoka kwa wakiukaji wa sheria za barabarani hasa kutokana na kupokea mishahara midogo.
Mmoja wa wakazi wa Kinshasa anasema kuwa wakati Roboti hizo zinaposimamisha magari, unaona madereva wanatii huku watu wakivuka barabara bila matatizo yoyote.
Wengi wanalaumu polisi wa trafiki kwa kuwahangaisha . Wanataka Roboti waachwe zifanye kazi hiyo ya polisi.
Roboti hizo zina urefu wa mita 2.5 na zilianza kutumika mwezi Juni mwaka jana katika barabara yenye shughuli nyingi sana mtaa wa Lumumba Boulevard.
Roboti hiyo husema kwa sauti kubwa: ''Madereva mnahitaji kutoa nafasi kwa watu kuvuka barabara,'' huku ikiinua mkono mmoja ukionyesha taa nyekundu na kijani kama ishara ya kuenda au kusimama.CHANZO BBC SWAHILI

 

No comments:

Post a Comment