Friday 28 February 2014

TOTAL YAZINDUA AWANGO KUMALIZA TATIZO LA UPATIKANAJI WA UMEME


Mgeni rasmi, Waziri wa Nishati na Madini, Mh. Prof. Sospeter Muhongo akihutubia wageni waalikwa (hawapo pichani) waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa bidhaa za AWANGO uliofanyika ndani ya hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam, usiku wa jana. Waziri Muhongo aliwapongeza TOTAL kwa juhudi wanazozifanya kusaidia jamii ya Watanzania kupata chanzo cha nishati kitakachowaletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Pembeni ni baadhi ya bidhaa hizo zinazotumia nishati ya jua.
Waziri wa nishati na madini Prof. Sospeter Muhongo (kulia), mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa bidhaa zinazotumia nishati ya jua kuzalisha umeme zinazojulikana kama AWANGO, wa kwanza kushoto ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mh. Marcel Escure pamoja na Mkurugenzi mkuu wa TOTAL nchini Tanzania Bw. Stephane Gay wakishuhudia tukio mojawapo katika hafla hiyo.
Kikundi cha burudani kikionyesha umahiri wa kutoa burudani kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) kuashiria uzinduzi rasmi wa AWANGO. AWANGO ni bidhaa zilizo chini ya Mradi wa ‘Total Access to Solar’ ulioanzishwa na kampuni ya TOTAL mwaka 2010 kusaidia kutatua tatizo la upungufu wa nishati kwa nchi zinazoendelea ukiwalenga watu wa kipato cha chini hasa wa vijijini na pembezoni mwa miji.
Meneja wa Maswala ya Kisheria na Ushirika wa kampuni ya TOTAL Tanzania Bi. Marsha Msuya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa bidhaa za AWANGO zilizo chini ya mradi wa TOTAL unaojulikana kama ‘Total Access to Solar’ (TATS) wenye lengo la kutatua tatizo la ukosefu wa umeme nchini Tanzania kwa jamii ya watu wa kipato cha chini. Bi. Marsha alisema kuwa bidhaa hizo zitafika katika mikoa yote nchi nzima.

No comments:

Post a Comment