Friday 7 March 2014

Mnyika atishia kuwataja vigogo

Wakati huohuo, Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika ametishia kuwataja kwa majina vigogo wa Serikali na CCM aliosema wako nyuma ya ‘kashfa’ kuhusu mgogoro huo ili waweze kuhojiwa kwa umma iwapo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo hatajitokeza kufafanua kauli alizozitoa bungeni kutuhumu IPTL.
Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo (Chadema), alisema hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, akimtuhumu Waziri Muhongo kwa kudai bungeni Mei 25, 2013 kuwa yeye hakutumwa wizarani kupekua mafaili ili kufuatilia mlolongo wa kesi za IPTL.
Alisema anachukua hatua hiyo kwa kuzingatia kwamba madaraka na mamlaka ni ya wananchi... “Serikali inafanya kazi kwa niaba ya wananchi; hivyo pale Serikali inapochelewa kuchukua hatua kutokana na udhaifu, uzembe, ufisadi au uongo, ni muhimu wananchi wakashiriki kutaka uwajibikaji.”


No comments:

Post a Comment