Friday 7 March 2014

Wanadiplomasia watimuliwa Venezuela

Serikali ya Venezuela imemtimua Balozi wa Panama na wanadiplomasia wengine wakati huu kukiwa na maandamano ya upinzani nchini humo.

 

 Rais wa Venezuela,Nicolas Maduro

Maafisa hao walipewa saa 48 kuondoka nchini Venezuela.
Hatua hii imekuja siku moja baada ya Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi na Panama.
Takriban watu 20 wameuawa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali ya Venezuela mwezi uliopita.
Maduro ameishutumu Panama kupanga njama za kuiangusha serikali yake.
Raia wa Venezuela kwa muda mrefu wamekua wakilalamikia ongezeko la vitendo vya uhalifu, kupanda kwa gharama za maisha na ukosefu wa bidhaa muhimu.

 

No comments:

Post a Comment