Tuesday, 11 March 2014

Askofu Mtetemela awatuliza wananchi

Dodoma. Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Donald Mtetemela amewahakikishia Watanzania kuwa Katiba itapatikana kwa wakati.
Hata hivyo, amesema kuna haja kwa Watanzania wa dini zote kuliombea Bunge Maalumu la Katiba lifanye mambo kwa kumshirikisha Mwenyezi Mungu ili mchakato wa Katiba uende vizuri.
Askofu Mtetemela, ambaye ni mmoja wa mjumbe wa Bunge hilo, alitoa ushauri huo jana kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Alisema kuyumba kwa Bunge la Katiba kwa sasa kunatokana na misimamo ya vyama vya siasa na kwamba kitendo hicho kimesababisha kuchelewa kwa kazi ya msingi.
“Mambo ya misimamo hayawezi kuzuilika na wala si kosa kila kikundi kuwa na msimamo wake, lakini kinachotakiwa ni wajumbe kufuta mambo ya vyama vichwani mwao na hasa pale panapokuwa na hoja ya msingi,” alisema kiongozi huyo wa kiroho.
“Watanzania waendelee kutuombea kwa nguvu zote. Sina shaka tutatoka hapa tukiwa wamoja kwa sababu tunaimba wimbo mmoja wa kutaka kitu kizuri mbele yetu,” alisisitiza Askofu Mtetemela.
Askofu Mtetemela alisema kuwa katika hatua za awali kulikuwa na misukosuko mikubwa ndani ya Bunge, lakini sasa kuna mwelekeo wa kuridhisha kutokana na wajumbe kuelewa wajibu wao katika mchakato huu.

 

Bunge Maalumu la Katiba sasa vululu vululu

 

Dodoma. Matarajio ya Bunge Maalumu la Katiba kukamilisha kanuni kwa maridhiano yaliyeyuka tena jana huku mambo ndani ya ukumbi yakionekana kuwa vululuvululu kwa baadhi ya wajumbe kuzungumza nje ya utaratibu na wengine kurushiana vijembe.
Baadhi ya wajumbe waliamua kutoleana lugha chafu na kuweka kando hoja za msingi zinazowafanya watofautiane na kuchelewesha kazi ya kuandika Katiba Mpya.
Hali ilichafuka mchana wakati wajumbe walipokutana kupitisha kanuni baada ya mmoja wao, Felix Mkosamali kuomba mwongozo kwa Mwenyekiti wa muda, Pandu Ameir Kificho. Hata hivyo, Kificho alimtaka kukaa chini kwa muda kwa maelezo kuwa wajumbe waliofika katika kikao hicho walikuwa wachache, hivyo mwongozo wake kama ulikuwa unahitaji majibu ingekuwa vigumu kutolewa.
Baada ya muda alisimama, James Mbatia na kuomba mwongozo, akihoji sababu za kutaka kuanza kikao cha kupitisha kanuni hizo wakati wajumbe hawajapewa vitabu vya rasimu ya kanuni zenyewe.
“Mwenyekiti ulitangaza asubuhi kuwa tutagawiwa kanuni kabla ya saa tisa lakini hadi sasa tunataka kusomewa kanuni wakati hatujagawiwa kanuni hizo,” alihoji Mbatia.
Kificho alitoa ufafanuzi kuwa kanuni hizo zilikuwa bado zinadurufiwa na kuwataka wajumbe wawe na nidhamu kwani anapotangaza wanapiga kelele.
Ghafla alisimama Mkosamali tena na kuwasha kipaza sauti na kuhoji kitendo cha mwenyekiti huyo kumpa Mbatia nafasi ya kutoa mwongozo wakati yeye amenyimwa... “Mwenyekiti hivi unaongozaje kikao, inakuwaje mimi nikuombe mwongozo uninyime na mwenzangu umpe? Mwenyekiti nakuheshimu sana, lakini sijui unatumia kanuni ipi kutoa nafasi kwa mjumbe wakati mimi ulinizuia nisiseme,” alihoji Mkosamali.
Baada ya kauli hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Hawa Ghasia aliwasha kipaza sauti na kwa sauti ya juu alisema “Mtoto mdogo hana adabu.” Kauli hiyo iliibua hasira za Mjumbe mwingine, Moses Machali ambaye naye aliwasha kipaza sauti na kumjibu: “Kubwa jinga halina adabu,” kauli iliyoibua miguno ndani ya Bunge.
Hata hivyo, licha ya Mwenyekiti kutoa onyo kwa kauli hizo kwamba hazifai, Mkosamali alisimama katika sehemu yake na kusema kuwa hakuna mtoto mdogo na kwamba tangu lini mtoto aliishinda CCM.
Chanzo cha tatizo
Chanzo cha mvurugano huo ambao wiki iliyopita kidogo usababishe ngumi kurushwa bungeni, ni mfumo wa upigaji kura katika kupitisha ibara za rasimu, ambao jana uliendelea kuwagawa wajumbe na kufanya ukumbi huo kuonekana kama eneo la mzaha.
Kauli za ‘ndiyoooo’, ‘hapanaaaa’ na vitendo vya kugonga meza viliongezeka katika kipindi cha asubuhi baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kuandaa Kanuni, Profesa Costa Mahalu kuwaleza wajumbe kuwa kamati yake haijafikia mwafaka wa ama iwe kura za siri au wazi na kwamba suala hilo limerejeshwa kwa wajumbe wenyewe.

 

Meli ya Korea Kaskazini yanaswa Libya

Wakuu nchini Libya, wamesema kuwa wameikamata meli moja iliyokuwa na bendera ya Korea Kaskazini, ikiwa na shehena haramu ya mafuta katika bandari inayodhibitiwa na waasi.

 

Msemaji wa shirika la kitaifa la mafuta, amesema kuwa meli hiyo ilisimamishwa ilipokuwa ikijaribu kungoa nanga na kwa sasa inasindikizwa katika bandari inayodhibitiwa na serikali ya Libya.
Maafisa wa serikali ya Libya waliisimamisha Meli hiyo ya Korea Kaskazini ilipokuwa ikiondoka kutoka bandari inayodhibitiwa na waasi siku ya Jumatatu ikiwa imesheheni mzigo usio rasmi wa mafuta ghafi.
Jeshi la nchi hiyo limethibitisha tukio hilo.
Waasi wa zamani wanaotaka kuitenga eneo la Libya Mashariki, wamekuwa wakimiliki bandari ya Al-Sidra na vituo vingine muhimu vya kuuzia bidhaa nje katika eneo hilo tangu Julai mwaka uliopita.
Mnamo siku ya Jumamosi, walianza kupakia shehena ya mafuta yasiyosafishwa ndani ya meli hiyo ya Korea Kaskazini iitwayo Morning Glory, iliyokuwa imetia nanga katika bandari ya Al-Sidra.

Viongozi walaani wizi wa mafuta

Kiwanda cha mafuta nchini Libya
Siku ya Jumatatu jeshi la wanamaji lilizuilia meli hiyo ilipokuwa ikiondoka bandarini, huku amri ikitolewa ielekezwe hadi katika bandari inayodhibitiwa na serikali.
Chama kikuu cha kisiasa nchini humo cha General National Congress, GNC, kimethibitisha kuzuiliwa kwa meli hiyo.
Runinga ya taifa Nchini Libya Al-Nabaa pia imeripoti tukio hilo kwa undani.
Walid al-Tarhuni, ambaye ni msemaji wa zamani wa kundi la waasi ambalo limekuwa likidhibiti bandari hiyo, ameiambia runinga ya Al-Nabaa kuwa meli hiyo ya mizigo ilikuwa ikielekea katika bandari ya Zawiyah, kilomita 50, Magharibi mwa mji mkuu Tripoli, kupakua mafuta hayo.
Utawala wa Washington umesema kuwa umeshangazwa na tukio hilo na kukariri kuwa mafuta inayotoka Libya ni mali ya raia wa nchi hiyo na wala sio ya makundi fulani.

 

Malaysia yazidisha kasi kutafuta Ndege 

Zoezi la kutafuta ndege ya abiria ya Malaysia limeendelea kushika kasi baada ya kuwepo kwa hali ya sintofahamu na wasiwasi mwingi kutoka kwa ndugu za watu waliopotea wakiwa katika ndege hiyo.

 

Ndugu wa waliopotea wameelezwa kuwa wakae tayari kupata habari mbaya

 Mamlaka nchini Malaysia zinasema wameongeza mipaka ya eneo la utafutaji, mara mbili Zaidi, huku China ikiwa imepeleka mitambo 10 ya satelaiti kwa ajili ya kusaidia kutafuta ndege hiyo.

Mkuu wa Idara ya anga Azharuddin AbdulRahman amewaambia waandishi wa habari kuwa eneo la kusaka ndege hiyo limeongezeka mara mbili kutoka maili 50 za baharini kunakosemekana ndege ilipotelea mpaka maili 100.
Ndege iliyokua imebeba watu 239 ilipotea bila kutoa taarifa yeyote na hakuna dalili yeyote mpaka sasa ya kupatikana kwa mabaki ya ndege hiyo.

 

Monday, 10 March 2014

Syria yawanyima chakula wakimbizi

 

Serikali ya Syria inadaiwa kutumia mbinu zisizofaa kuwanyima chakula, raia, wasio na hatia na ambao pia ni wakimbizi.
Shirika la kimataifa la Amnesty International linasema kuwa serikali inatumia njia ya kuwanyima chakula raia kama silaha dhidi ya wakimbizi ambao wako katika kambi za wakimbizi na ambao wanahitaji msaada wa dharura.
Kwa mujibu wa shirika hilo wakimbizi 128 wamefariki katika kambi ya wakimbizi ya Yarmouk mjini Damascus kutokana na kukosa chakula.
Shirika hilo linasema kuna hali ngumu ya kibinadamu inayowakabili wakimbizi hao.
Shirika la Amnesty linasema kuwa familia nyingi zimelazimika kutafuta chakula katika jaa za takataka na kuhatarisha maisha yao.
Kulikuwa na ripoti za mapigano mapya kuzuka karibu na kambi hiyo mapema wiki hii.
Mwandishi wa BBC Rami Ruhayem, anasema kuwa mapigano yalisitishwa kwa muda ili kuweza kuwafikishia chakula wakimbizi mjini Damascus
Kambi ya Yarmouk ambayo inawahifadhi wakimbizi 17,000 hadi 20,000 wa kipalestina na wengine raia wa Syria, imeshuhudia vita vikali mno katika siku za hivi karibuni.
Kambi yenyewe imekuwa bila stima tangu Aprili mwaka 2013 na nyingi ya hospitali za mji huo zimefungwa baada ya kukosa vifaa muhimu.

 

POLISI YAAGIZWA KUSAKA DAWA ZA SERIKALI ZENYE NEMBO YA MSD KATIKA MADUKA YANAYOUZA DAWA BARIDI NCHINI KOTE.

Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini ambaye ni Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka akisindikizwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya MSD (Kulia) Prof. Idris Alli Mtulia na Kushoto kabisa ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Madawa nchini (MSD) Bw. Cosmas Mwaifwani wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kituo cha kuhifadhi na usambazaji dawa Wilayani Muleba Mkoani Kagera. 

Kituo kipya cha muda cha Kutunza na Usambazaji Dawa cha Bohari Kuu ya Madawa (MSD) kilichozinduliwa Jumamosi na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (Akimwakirisha Makamu wa Rais Dk. Mohamerd Ghalib Bilal ) kilichopo eneo la Mahalahala Wilayani Muleba Mkoa wa Kagera. 
MKurugenzi wa MSD Kanda Makao Makuu Dar es salaam Mr Tell akiteta jambo na Meneja wa MSD Kanda ya Mwanza Tabula Byekwaso kabla ya kuanza kwa sherehe za uzinduzi wa Kituo kipya cha muda cha Kutunza na Usambazaji Dawa cha eneo la Mahalahala Wilayani Muleba March 8 Mwaka huu.
Wanawake ambao ni wananchi wa Wilaya ya Muleba na maeneo ya jirani na Kituo kipya wakijumuika na baadhi ya watumishi wa MSD kusakata dansi la Bendi ya Muziki ya Kakao eneo la uzinduzi Mahalahala Wilayani Muleba.
Waibaji na wacheza show wa Bebdi ya Kakao wakitumbuiza kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo kipya cha MSD eneo la Mahalahala Muleba.
Viongozi Jukwa Kuu wakishiriki kusakata rumba la Kakao Bandi
Afisa Habari wa MSD Makao Makuu (Mwenye Kipeperushi cha Bendera ya MSD) na Baadhi ya watumishi wakifuatilia kwa umakini shughuli za uzinduzi wa Kituo kipya 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Madawa nchini (MSD) akitoa taarifa fupi ya MSD kwenye sherehe za uzinduzi wa kituo kipya.
Zamu ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Prof. Idris Alli Mtulia akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Kituo hicho.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk Stephen Kebwe Aliyemwakirisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamerd Ghalib Bilal akihutubia viongozi, watumishi wa MSD na wananchi wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha MSD Wilayani Muleba
Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka  ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akitoa hotuba ya shukurani za wananchi wa Wilaya ya Muleba na Mkoa wa Kagera kwa kuzinduliwa kwa kituo kipya cha MSD Wilayani Muleba.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali ya uzinduzi wa kituo kipya cha MSD Muleba.
Kakao Bandi wakiwa kazini kutumbuiza wakati wa sherehe 
Baadhi ya wanawake wakifuatilia tukio la uzinduzi 
Kazi ni moja tu kushambulia ndani ya viwanja vya uzinduzi wanamuziki wa Kakao Bandi.
"Haya Mheshimiwa Mbunge sasa nakata utepe kuzindua rasmi usambazaji dawa za serikali ulio chini ya MSD" ni Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe akishuhudiwa na Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Tibaijuka (Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini)  
"Haya tupige makofi kwa pamoja kuashiria kukubali uzinduzi huu" Naibu Waziri Dk. Kebwe (Kulia), Waziri Prof. Tibaijuka (Katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu MSD Bw. Mwaifwani
Meneja wa MSD Kanda ya Mwanza Tabula akiwa na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Prof. Tibaijuka ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Prof. Mtulia (Mwenye suti) wapili Kulia, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe (Nyuma mwenye suti) na Mkurugenzi MSD Kanda Makao Bw. Tell (Mwenye miwani aliyevaa shati nyeupe nyuma) 
Ramani kuonyesha Mfumo wa Usambazaji Dawa kutoka MSD kwa kauli mbiu yake kufikisha dawa moja kwa moja hadi vituo vya kutolea huduma za afya ikiwa ni Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya na Teule, Mkoa na Rufaa maeneo yote nchini.
Baada ya kumalizikehe kwa sherehe za uzinduzi Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini alianzisha maandamano ya Amani kuunga mkono juhudi za serikali kufikisha huduma ya dawa na vifaa tiba kupitia Bohari Kuu ya Madawa (MSD) nchini kote ili kupunguzi vifo vya mama na watoto, mapambanaona ugonjwa  wa UKIMWI na Malaria.
Na Peter Fabian.
ALIYEKUWA MULEBA.

MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal ameiagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kufanya msako endelevu ili kuwafichua, kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaopatikana na Dawa za Serikali kinyume cha taratibu na sheria zilizopo.

Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Stephen Kebwe (MB) wakati wa ufunguzi rasmi wa Kituo cha Kutunza na Usambazaji Dawa (Bohari ya MSD) cha muda kilichopo eneo la Mahalahala kwenye Hospitali inayojengwa ya Wilayani Muleba juzi alisema wizi na upotevu wa dawa hizo zinazotolewa na serikali hufanywa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.

Alieleza kwamba Kituo cha Muleba (Bohari ya Madawa ya MSD) cha muda kitakuwa na jukumu kubwa la kusambza dawa na vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali na Vituo vya Afya katika maeneo yote ya Wilaya za Mikoa ya Kagera (Vituo 270 ) na Geita (Vituo 64) kuanzia mwezi julai mwaka 2013 mfumo huu wa usambazaji dawa ulianza kabla ya kufunguliwa rasmi.

Makamu wa Rais Dk. Katika hotuba hiyo ameipongeza Bohari Kuu ya Madawa (MSD) nchini kwa kuanzisha utaratibu wa kuweka alama ya Government Of Tanzania (GOT) katika dawa zinazosambazwa na kusema kuwa hatua hiyo itasaidia dawa za serikali kutambulika kiurahisi kwa wananchi pamoja na kuthibiti wauzaji wa maduka ya dawa baridi wanaopelekewa zinazoibiwa na watumishi wa serikali.

“Lengo kubwa la kufunguliwa kituo hichi ni kupunguza vifo vya akina mama na watoto, kupambana na ungonjwa wa UKIMWI na Malaria ikiwa ni kuanza kutumia mfumo wa fikisha dawa karibu na wananchi na kwa wakati ili kufanikisha lengo mahususi la serikali ya awamu ya nne huku ufatiliaji wake uwe chini ya usimamizi wa karibu na matumizi ya dawa zinazosambazwa kwenye vituo vya huduma ” alisisitza

Kwa upande wake Naibu Waziri Dk. Kebwe amesikitishwa na taarifa ya kasi ya wizi na upotevu wa dawa zinazopelekwa na serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) katika Wilaya za Ngara, Kerwa, Biharamulo na Muleba huku akizipongeza Wilaya za Karagwe na Bukoba vijijini kwa kuweka jukumu la udhibiti wizi na upotevo wa dawa hizo kutoka kwa watumishi wasio waadilifu.

Dk. Kebwe ameungana na Makamu wa Rais Dk. Bilal kuzitaka Kamati za ulinzi na usalama za Mikoa ya Kagera na Geita na zile za Wilaya kwa kushirikiana na Wakurugenzi na Wenyeviti wa Halmashauri zote kufatilia kwa ukaribu huku akitaka taarifa za upokeaji dawa na utolewaji kwa wananchi utolewe kwenye Vikao vya Kamati ya Ushauri na Maendeleo (RCC) za Mikoa yote.

“Tusikubaliane na wajanja wachache wa Idara za Afya kutumia mwanya wa kuiba dawa na kuziuza kwenye maduka waliyoanzisha na kisha kujinufaisha kwa kununua magari, kujenga vyumba za kifahari nasi kuwashangilia eti muda mchache jamaa ana gari zuri ambapo makusanyo ya mapato kutoka vituo vya afya kuonyesha ni asilimia 50 tu huku zingine zikiliwa na wajanja wachache” alisema.

Dk. Kabwe alisema kuwa Wizara yake itatumia bilioni 6 kwa mwaka katika Dawa zote zitakazotolewa na kituo hicho na kila mwezi kitasambaza dawa za kiasi cha shilingi milioni 150 huku Bajeti ya Wizara ikionekana kutumia Bilioni 80 za Dawa, Vifaa tiba na Vitenganifu na kupitia kituo hicho ndani ya siku 14 Hospitali na Vituo vya Afya vitapeka oda na kupatiwa dawa.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Porfesa Idrisa Mtulia kuzinduliwa kwa kituo hicho ni mkombozi mkubwa wa wananchi wa Mkoa ya Kagera na Mkoa wa jirani wa Geita na Wilaya zake zote ambapo kitawezesha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na viunganifu vya kutolea huduma ya afya kwa Bohari ya madawa kufikisha haraka huduma zake kwa wateja.

Prof. Mtulia alisema kwamba pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili MSD itahakikisha inashirikiana na serikali na wadau wengine kuendelea kutoa huduma bora na kufikisha dawa zenye ubora na bei nafuu wakati wote kwa manufaa ya watanzania wote  huku akihimiza Halmashauri zote nchini kukunua dawa kutoka MSD kwa kutumia vyanzo vyake vingine vya fedha.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) nchini Cosmas Mwaifwani alisema kwamba kutokana na ukubwa wa Kanda ya Ziwa na idadi kubwa ya wingi wa watu zaidi ya milioni 13 kutokana na matokeo ya Sensa ya mwaka 2012 kuwepo na malalamiko ya wadau mbalimbali juu ya huduma za MSD Kanda ya Mwanza kutokidhi kwa wakati huduma ya utoaji wa dawa.

Kaimu huyo alieleza kuwa imefungua kituo hicho cha muda kuhakikisha upatikanaji na usambazaji wa Kituo cha Muleba kinafanikisha lengo la MSD na kupunguza usumbufu wa Mkoa wa Kagera kufata huduma hiyo Jijini Mwanza na Kanda ya Tabora ambapo ilionekana kuchelewesha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba vyenye ubora na kwa bei nafuu kwa watanzania wote.

“Ufunguzi wa Kituo hiki cha usambazaji dawa Mkoani Kagera na Mkoa wa jirani wa Geita ni mchango mkubwa wa utekelezwaji wa Malengo ya Millenia hususani kupunguza vifo vya mama na watoto na kupambana na Ukimwi na Malaria ambayo imekuwa ni magonjwa ya mlipuko katika maeneo mengi ya Wilaya za Muleba ” Alisema Mwaifwani.
Mbunge wa Muleba Kusini Porfesa Anna Tibaijuka ambaye ni Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwahakishia Naibu Waziri Dk. Kebwe na uongozi wa MSD kuwa eneo la Ekhali 5 zilizotolewa na Halmashauri Wilaya ya Muleba linaachwa wazi ili kutoa nafasi kwa MSD kujenga Ofisi kuu na Maghala ya kuhifadhiwa dawa Mkoani humo.

“Kituo hiki ni wajibu wetu kukilinda na kukitunza vizuri ili kiendelee kutoa huduma, lakini Mkurugenzi wa Halmashauri naomba utumia sheria za ardhi zilizopo kuhakikisha unawaondosha watu wanaovamia eneo tulilotenga kwa ajili ya shughuli za MSD hili ni agizo natoa kama Waziri nila serikali siyo langu kama Mbunge wa Jimbo hili” alisisitiza.

Mbunge huyo aliongeza kuwa kutokana na waathilika wakubwa ni Kimama na watoto pamoja na Wilaya hiyo kukubwa na magojwa ya mlipuko hususani Malaria ambayo yalipelekea serikali na Wizara ya Afya kutuma wataalamu na kufanya utafiti kisha kuanzisha mkakati wa kupulizia dawa ya Ukoko kwenye nyumba za Wilayah ii ili kudhibiti ugonjwa huo uliokuwa ni janga kwa wananchi

Profesa Ibrahim Lipumba aifunda Chadema Dar

 

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetakiwa kuweka kando tofauti za kisiasa na kuunganisha nguvu zao, hasa katika kipindi hiki ambacho taifa lipo katika mchakato wa uundaji wa Katiba Mpya.
Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba alipokuwa akifungua mkutano wa baraza kuu la chama hicho.
Alisema kuwa chama hicho chenye wabunge wengi kinapaswa kutafakari na kuweka kando itikadi za vyama na kuangalia mustakabali wa nchi katika kipindi muhimu.
“Ningependa kuwashauri Chadema kama chama chenye wawakiishi wengi bungeni kinapaswa kuweka kando tofauti za kisiasa na kuunganisha nguvu katika kwa kuangalia masilahi na mustakabali wa taifa,” alisema
“Licha ya changamoto tulizonazo hakuna sababu ya kukata tamaa mapema kiasi hiki, tunapaswa kuondoa tofauti zetu za kisiasa a.”
Kauli hiyo ya Lipumba inakuja kutokana na vuguvugu la mgogoro ulioibuka hivi karibuni ndani ya Chadema ambao ulisababisha aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe kuvuliwa nafasi zake zote za uongozi.
Uamuzi huo pia ulimkumba aliyekuwa mjumbe wa Kamati kuu ya Chama hicho Dk Kitila Mkumbo na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.