Syria yawanyima chakula wakimbizi
Serikali ya Syria inadaiwa kutumia mbinu zisizofaa kuwanyima chakula, raia, wasio na hatia na ambao pia ni wakimbizi.
Shirika la kimataifa la Amnesty International
linasema kuwa serikali inatumia njia ya kuwanyima chakula raia kama
silaha dhidi ya wakimbizi ambao wako katika kambi za wakimbizi na ambao
wanahitaji msaada wa dharura.Shirika hilo linasema kuna hali ngumu ya kibinadamu inayowakabili wakimbizi hao.
Shirika la Amnesty linasema kuwa familia nyingi zimelazimika kutafuta chakula katika jaa za takataka na kuhatarisha maisha yao.
Kulikuwa na ripoti za mapigano mapya kuzuka karibu na kambi hiyo mapema wiki hii.
Mwandishi wa BBC Rami Ruhayem, anasema kuwa mapigano yalisitishwa kwa muda ili kuweza kuwafikishia chakula wakimbizi mjini Damascus
Kambi ya Yarmouk ambayo inawahifadhi wakimbizi 17,000 hadi 20,000 wa kipalestina na wengine raia wa Syria, imeshuhudia vita vikali mno katika siku za hivi karibuni.
Kambi yenyewe imekuwa bila stima tangu Aprili mwaka 2013 na nyingi ya hospitali za mji huo zimefungwa baada ya kukosa vifaa muhimu.
No comments:
Post a Comment