Obama amualika Waziri Mkuu wa Ukraine
Rais wa Marekani Barrack Obama, amemualika waziri
mkuu wa Ukraine, Arseniy Yatsenyuk, mjini Washington kwa mashauriano
kuhusiana na mzozo unaokumba taifa lake.
Ikulu ya White House, imesema kuwa mkutano huo
utakaofanyika siku ya Jumatano, utaangazia, mbinu za kutafuta suluhisho
la amani, kuhusiana na operesheni za kijeshi zinazoendesha na jeshi la
Urussi katika eneo la Crimea.Waandishi wa habari wanasema kuwa mualiko huo ni ni ishara thabiti kuwa Marekani inaunga mkono utawala wa mpito wa Kiev.
Wakati huo huo, jamii ya kimataifa inaendelea kuishinikiza utawala wa Moscow, kuondoa wanajeshi wake katika eneo la Crimea.
Chansella wa Ujerumani, Angela Merkel, amemueleza rais wa Urussi, Vladimir Putin, kutilia maanani kuwa kura ya maoni kuhusu ikiwa eneo hilo la Crimea, litajiunga na Urussi inakiuka sheria na ni haramu.
Khodorkovsky apinga utawala wa Moscow
Amewaambia maelfu ya watu waliofurika katika medani ya Uhuru kuwa serikali ya Urussi inawahadaa raia wake kwa kuwahusisha waandamanaji mjini Kiew na watu wanaopinga utawala wake na raia wake.
Mikutano kama hiyo imefanyika katika sehemu kadhaa za nchi hiyo.
Nyingi zikiwa za amani lakini mjini Sevastopol, katika eneo la Crimea, raia wa Ukraine wanaozungumza lugha ya Kirussi waliwapiga watu wanaounga mkono serikali ya Ukraine.
Televisheni zilizo na makao yao mjini Kiev zimezuiliwa kurusha matangazo katika eneo hilo la Crimea.
No comments:
Post a Comment