TZ, Kenya lawamani kwa kukwamisha biashara A.Mashariki
Kilimanjaro. Tanzania na Kenya zinakwamisha
kuanza kazi kwa Kituo cha pamoja cha Mpakani (OSBP) cha Holili wilayani
Rombo, ambapo ujenzi wake ulikamilika tangu Desemba mwaka jana.
Kituo hicho ni kwa ajili ya ukaguzi wakati wa
kuvuka mpaka wa Tanzania na Kenya, ambapo wananchi wa nchi hizo mbili
watakaguliwa katika kituo kimoja badala ya viwili kama ilivyo sasa.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mipaka wa Taasisi ya
Trademark East African (TMEA), Theo Lyimo alisema ujenzi wa kituo hicho
umefadhiliwa na taasisi hiyo kwa Dola 5.7 milioni (Sh. 9.1 bilioni).
Lyimo aliwaeleza waandishi wa habari wa Tanzania
na Kenya waliotembelea vituo vya Holili na Taveta. “Vituo hivi vikianza
kazi kama mtu anatoka Tanzania kwenda Kenya atakaguliwa Taveta upande wa
Kenya, ambako katika kituo hicho kutakuwa na maofisa wa nchi hizo mbili
wa TRA, Uhamiaji na Afya ,” alisema.
Lyimo alisema jengo jingine linajengwa katika
mpaka huo lipo katika eneo la Taveta upande wa Kenya litakalogharimu
Dola 6.7 milioni (Sh.10.7 bilioni ) ambalo litakamilika katika kipindi
cha miezi mitatu ijayo.
Alisema pia kwa wasafiri wanaotoka Kenya kwenda
Tanzania watakaguliwa katika eneo la Holili upande wa Tanzania ambako
pia kutakuwa na maofisa wa nchi hizo mbili.
No comments:
Post a Comment